Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Friday, August 18, 2017

Walimu 15 wafutwa vibarua Mkoani Dodoma.

Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Chamwino, Dodoma, imewafukuza kazi walimu 15 wa shule za msingi na sekondari wilayani humo, kwa kosa la utoro kazini akiwamo ambaye ametoroka kazini kwa siku zaidi ya 400 na kukimbilia kufundisha shule binafsi.
Mashauri 18 ya utoro yalipokelewa na tume hiyo kutoka kwa walimu wakuu na mwajiri wa walimu ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri kutokana na kuwapo kwa tabia ya walimu kutohudhuria kazini kwa muda mrefu na kuathiri taaluma ya elimu ndani ya wilaya hiyo.
Kaimu Katibu Msaidizi wa Tume hiyo wilaya ya Chamwino, Khalidi Shabani amesema tatizo la utoro kwa walimu limeendelea kukua katika wilaya hiyo kutokana na walimu watoro kulindwa na baadhi ya viongozi wanaozuia hatua stahiki kuchukuliwa dhidi yao.

0 comments:

Post a Comment