Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa African news tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Jim Media Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Labels

Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Monday, November 13, 2017

HUU NDIO UJIO WA ALBAM MPYA YA DIAMOND IITWAYO "A BOY FROM TANDALE"



Ni alipokuwa akifanya mazungumzo baina ya Salim Kikeke wa shirika la Utangazaji la Uingereza BBC na Msanii Diamond Platnumz Alipotembelea BBC LONDON.

 Albam hiyo mpya imewajumuisha wasanii kutoka maeneo mbalimbali duniani akiwamo Rick ross, Young Killer, na Davido

Wednesday, November 1, 2017

Aslay avuta ndinga mpya itizame hapa.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay Isihaka ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Natamba' amefunguka na kushukuru uongozi wake mpya kwa kufanikisha yeye kuweza kupata ndinga mpya aina ya BMW. 
Aslay ambaye ndani ya muda mfupi ameweza kuachia nyimbo zaidi ya 10 na ngoma hizo nyingi kufanya vizuri na kupokelewa vyema na wananchi jambo ambalo limeweza kufungua milango kwa msanii huyo kuweza kupata show nyingi na mafanikio mbalimbali. 

"Alhamdulillah Asantee Mungu kwa hiki ulichonipa naishukuru management yangu Chambusso na Mxcarter, nakupenda Mama yangu kokote ulipo kila hatua dua 'new car' Umma unaongea" alindika Aslay kupitia mtandao wake wa Facebook. 


Aslay Isihaka kwa mara ya kwanza kuanza kumiliki gari yake alizawadiwa na uongozi wake wa kwanza wa Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake mwaka 2015

Tuesday, October 31, 2017

Alichokiandika Jaguar baada ya Uhuru Kenyatta kutangazwa Rais wa Kenya.



Msanii Jaguar wa Kenya na pia Mbunge wa jimbo la Starehe County ya mjini Nairobi kupitia muungano wa chama cha Jubilee, amempongeza Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena katika kiti cha Urais katika uchaguzi wa marudio ambao umefanyika wiki iliyopita.

Kupitia mtandao wa Twitter, Jaguar ameandika, “Congratulations @UKenyatta on your reelection. I thank all who voted and equally expressed their democratic right. Let’s maintain peace.”




Rais Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo (IEBC), Wafula Chebukati kupata kura 7,483,895 sawa na asilimia 98, mpinzani wake Raila Odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa naasilimia 0.96.

Jumla ya wananchi 7,616,217 walipiga kura katika uchaguzi huo kati ya watu milioni 19.6 waliojiandikisha kupiga kura.

Wednesday, October 25, 2017

Shahidi afichua mapya ya Kanumba

Kesi inayomkabili Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu', imeendelea leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo ushahidi wa upande wa utetezi uliokuwa ukisubiriwa umewasilishwa na kusomwa na Polisi Detective Sergeant Nengea aliyerekodi.


ushahidi huo kutoka kwa aliyekuwa Daktari wa Marehemu Steven Kanumba.

Katika ushahidi uliosomwa na Sergeant Nengea (ambaye mahakama imemtambua kama shahidi) ambao aliurekodi kutoka kwa Josephine Mushumbusi umedai kwamba "Marehemu alikua na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo, alikuwa anasikia maumivu katika ubongo na akili kuchoka".

Aidha ushahidi huo umekamilisha kesi hiyo siku ya leo lakini Wakili Kibatala ameiomba mahakama kumruhusu kumpatia nafasi ya kutoa hoja za ziada ambazo zitasaidia katika kufanya maamuzi juu ya kesi hiyo.

Hata hivyo Jaji Sam Rumanyika amesema kesho wazee wa baraza watakaa na kujadili kama Lulu ana hatia katika kesi hiyo inayomkabili au hana, na kusubiria kupanga siku ya hukumu.