
Makamu wa rais wa Zimbabwe aliyefukuzwa Emerson Mnangagwa amemtaka Rais Robert Mugabe kuheshimu maoni ya umma na kuachia ngazi, akiongeza kuwa atarejea nyumbani iwapo tu atahakikishiwa usalama wake.
Mnangagwa alikimbia Zimbabwe muda mfupi baada ya kufutwa kazi na Mugabe mapema mwezi huu.
Mzozo huo ulitokana na mvutano wa makundi ndani ya chama tawala cha ZANU-PF kuhusu nani atakayemrithi Mugabe.
Aidha, Mnangagwa amekataa mwito wa Mugabe wa kumtaka kurejea nyumbani kujadili hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa, akisema amemueleza rais huyo kwamba hatarejea hadi atakapokuwa na uhakika wa usalama wake.
Katika hatua nyingine, maveterani wa vita wenye ushawishi nchini humo, wameitisha maandamano ya dharura ya kumpinga rais Robert Mugabe, wakati bunge likijiandaa kumuondoa madarakani.
Mwenyekiti wa maveterani hao, Chris Mutsvangwa amewataka raia kwenda hadi kwenye makazi binafsi ya Mugabe, yanayojulikana kama Blue Roof, kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anayendelea kutengwa na watu, anaondoka haraka.
0 comments:
Post a Comment