
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema kuna aina nne za mambo yanayotishia usalama katika nchi za Afrika Mashariki.
Mambo hayo ni ya ugaidi, uharamia, majanga kama matetemeko ya nchi, pamoja na ya kisiasa. Balozi Mahiga alisema hayo juzi wakati akifunga mafunzo ya ‘Ushirikiano Imara 2017’, jijini Dar es Salaam, ambayo nchi za Afrika Mashariki zimeshiriki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Alisema licha ya tishio hizo, bado majeshi ya usalama yapo imara, na Tanzania mpaka sasa haijafikia hatua ambayo inatishia amani. Alisema kwa mara ya kwanza mazoezi hayo yamefanyika Tanzania, yanadumisha uzalendo na kubadilishana mawazo.
“Zoezi hili ni la muhimu sana na sehemu ya itifaki. Mwaka jana yalifanyika nchini Kenya. Leo ni fursa ya uongozi wa juu kabisa katika majeshi ya Afrika Mashariki kukaa pamoja na kufanya mazoezi pamoja na Tanzania tumekuwa wenyeji,” alisema Balozi Mahiga.
0 comments:
Post a Comment