Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameongoza mkutano wa wake wa kwanza
wa kamati kuu ya chama cha ZANU-PF, baada ya rais wa zamani Robert
Mugabe kujiuzulu wiki tatu zilizopita.
Mkutano huo uliofanyika kwenye makao makuu ya ZANU PF umeashiria mwanzo wa mkutano mkuu wa kawaida wa siku moja wa chama uliopangwa kufanyika kesho.
Mkutano huo uliofanyika kwenye makao makuu ya ZANU PF umeashiria mwanzo wa mkutano mkuu wa kawaida wa siku moja wa chama uliopangwa kufanyika kesho.
Ajenda za mkutano mkuu huo ni pamoja na kumthibitisha Bw. Mnangagwa
kuwa rais na katibu mkuu wa ZANU-PF, kutambuliwa kwake kama mgombea
urais wa chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika mwaka kesho, na
kuidhinisha kuwafukuza wanachama wanaosemekana kuwa kundi la G40 la mke
wa rais wa zamani Bibi Grace Mugabe. @cri
0 comments:
Post a Comment