Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi
kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwamba taasisi hiyo ndiyo
inayoshughulika na haki za watu na wasipofanya kwa uadilifu yapo
madhara makubwa kwa jamii na kutoka kwa wahalifu.

‘’Kamateni wahalifu wote wanaoingia kimagendo au wanaoingiza mizigo kimagendo hakuna mjadala kamateni na wafikisheni katika vyombo vya sheria ,’’amesema Dk Mwigulu.
Kwa mujibu wa Dk Mwigulu, Mikoa ya kaskazini mwa Tanzania inaongoza kwa kuingiza wahamiaji haramu na bidhaa kwa magendo kwasababu ipo mipakani hivyo kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi hizo.
‘’Ujenzi huu wa kituo cha polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama zaidi hivyo mimi nitachangia nondo 150 baada ya mifuko 450 ya cement kupatikana basi ujenzi uanze haraka iwezekanavyo na kituo kiwe cha hali ya juu kikubwa.’’ amesisitiza
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wilaya hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa polisi Christina Musyani amesema kuwa wilaya hiyo ina vituo vitatu pekee vya polisi ambavyo havitoshi na mazingira yake hayaridhishi.
Amesema wameamua kuanza ujenzi wa kituo hicho ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa sasa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta vituo vya polisi.
"Kwa kushirikiana na wananchi, Mbunge na halmashauri tumeamua kuanza ujenzi wa kituo cha kisasa ,’’ amesema Christina.
0 comments:
Post a Comment