Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.
Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.
"...prof muhongo ni rafiki yangu na nampenda sana, lakini kwa hili sitamsamehe, ajiassess aone kama anafaa kuendelea kuwepo na achukukue hatua haraka ya kuachia madaraka"
Rais Magufuli vilevile amevunja Bodi ya Ukaguzi wa Madini (TMAA) na kumsimamisha kazi ofisa mtendaji mkuu wake huku akiagiza dola,PCCB kuwachunguza wafanyakazi.
Muhongo anawakuwa Waziri wa tatu wa serikali ya Magufuli Kuondoshwa kibaruani akitanguliwa na Charles Kitwanga na Nappe Nnauye.
Kwa hatua hiyo Bunge la Jamhuri ya Muungano linaloketi Dodoma kwa vikao vya Bunge limeahirisha Hotuba ya bajeti ya wizara ya Nishati na Madini hadi siku ya jumatatu iliyotakiwa kusomwa kesho badala yake Wabunge watapokea na kuijadili hotuba ya bajeti ya wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi.
0 comments:
Post a Comment