Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Saturday, May 20, 2017

Trump awasili Saudi Arabia kukutana na Viongozi wa Kiislam

Rais Donald Trump afanya mazungumzo mafupi na Mfalme wa Saudi Salman Bin AbdulazizRais Donald Trump na mkewe Melania Trump wakilakiwa na Mfalme Salman mara baada ya kuwasili Saudi Arabia
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump wakilakiwa na Mfalme Salman mara baada ya kuwasili Saudi Arabia

Mfalme na familia ya Trump walitembea katika zulia jekudu wakati wakielekea kwenye ukumbi wa kifalme, katika mashukio ya ndege hapo uwanjani, ambapo walifanya mazungumzo mafupi.

Baada ya muda mfupi, Trump, akiwa na Mfalme wa Saudi waliondoka airport katika gari maalum, wakielekea mjini kupitia njia ambazo hazina msongamano wa magari.

Akiwa nchini Saudi Arabia, Rais Trump anatarajiwa kusaini mikataba minono ya silaha inayokisiwa kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 100. Katika ziara hiyo ya siku mbili, Rais Trump anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano wa mataifa zaidi ya 50 ya Kiarabu na Kiislamu juu ya mapambano dhidi ya itikadi kali katika Ukanda wa Mashariki ya Kati.
Katika mkutano huo mambo kadhaa yanatarajiwa kuchukua nafasi kubwa kujadiliwa ikiwa ni pamoja na kukua kwa ushawishi wa Iran katika ukanda huo, Vita nchini Syria na Vita dhidi ya kundi la kigaidi la ISIS.
Ziara hiyo itamfikisha Trump nchini Israel ambapo anatarajiwa kujadili mkataba wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015 kati ya mataifa yenye nguvu na Iran, Italy ambapo atakutana na Baba Mtakatifu nkabla ya kuelekea Brussels nchini Ubelgiji atakapohudhuria mkutano wa NATO.

0 comments:

Post a Comment