KUFUATIA uchaguzi uliofanyika jana Ijumaa nchini Iran, Rais aliyekuwa anatetea kiti chake kwa mhula wa pili Hassan Rouhani ametangazwa mshindi kwa asilimia 58.6 akimbwaga mshindani wake wa karibu Ebrahim Raisi aliyepata asilimia 39.8.
Ebrahim Raisi anayeungwa mkono na Kiongozi wa Kidini wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei, ni mmoja wa viongozi wa kidini mwenye msimamo mkali anayepinga vikali sera za kujongelea mataifa ya magharibi.
Uchaguzi huo ulikuwa mtihani kwa Rais Rouhani kufuatia sera yake ya mageuzi ambapo ameifanya Iran kuwa karibu na mataifa ya magharibi hadi kufikia kuingia mkataba na mataifa yenye nguvu juu ya mradi wake wa nyuklia.
Kwa matokeo hayo ni ishara ya wazi kuwa wananchi wa Taifa hilo la Kiislamu wamekubaliana na sera za Rais Rouhani. Sera hizo za kujongelea mataifa ya magharibi zenye lengo la kupunguza kutengwa na mataifa hayo pamoja na kupunguza kwa kiwango kikubwa kwa vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment