Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali.
Wengine waliokamatwa ni pamoja na madiwani wawili na viongozi wa Shirikisho la Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongsco) na baadhi ya viongozi wa dini. Hata hivyo, baada ya kufikishwa Polisi, waandishi waliachiwa kwa maelezo kuwa, walikamatwa kimakosa.
Kusanyiko hilo lilielezwa lilikuwa na lengo la kuwapa rambirambi wazazi waliofiwa na watoto katika ajali ya basi la Shule ya Msingi Lucky Vicent ya jijini hapa. Ajali hiyo ilitokea eneo la Rhotia, Karatu wakiwa katika safari ya kimasomo Mei 6 mwaka huu na kuua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo alisema mmoja kati ya viongozi wa Tamongsco, Kanda ya Kaskazini alikuwa na Sh milioni 18 kwa ajili ya kutoa rambirambi kwa wafiwa lakini ilishindikana baada ya kukamatwa na polisi waliofika shuleni hapo.
0 comments:
Post a Comment