Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoani
Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari
ya Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na
mwanafunzi wake darasani usiku.
Kasinge ametoa agizo hilo baada ya
kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga
ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.
“Kuanzia wanafunzi waliotimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya mtandao wa kutaka kumsaidia ama kupotosha ushaidi,” amesema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge.
Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya sanaa.
0 comments:
Post a Comment