
Na Tiganya Vincent, NZEGA
Madiwani
 katika Halmashauri za  Mkoa wa Tabora  wametakiwa kuepuka kujenga 
makundi miongoni mwao ambayo yamekuwa yakisababisha wananchi 
waliowachagua kuchelewa kupata maendeleo kwa sababu ya muda mwingi 
kushughulikia migogoro badala ya kutatua matatizo mbalimbali ya 
wananchi.
Hayo
 yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akifunga 
mafunzo ya siku nne ya Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora 
yaliyofanyika wilayani Nzega  kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu 
shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD) 
iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo (LGDG)
Alisema
 makundi yatawafanya washindwe kuwajibika vizuri na kujikuta miaka 
mitano ya uongozi wao inakwisha bila kuwafanyia chochote wananachi zaidi
 ya kupigania kuondoana katika uongozi badala kukazania maslahi ya 
wananchi.
“Nyie
 ndio mliko zamu sasa mkiendekeza makundi na migogoro isiyokwisha, 
mtajikuta zamu zenu zinamalizika hamjawafanyia chochote wananchi 
waliowachagua badala yake kupambana kila mnapokutana katika vikao vyenu 
….kila kikao itakuwa sisi hatumutaki fulani atuongoze au fulani fulani 
hatufai” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Bw.
 Mwanri aliongeza kuwa wakimruhusu Shetani wa namna hiyo apite kati yao 
hakuna tena kazi wala maendeleo kwa wananchi wao waliowachagua.
Alisisitiza
 kuwa viongozi wa aina hiyo wanakuwa wamekosa sifa ya kuendelea 
kuaminiwa na jamiii iliyowachagua tena kuwatetea wananchi katika 
matatizo yanayokwamisha maendeleo yao.
Mkuu
 huyo wa Mkoa aliwataka Madiwani wote washirikiane bila kujali itikadi 
za vyama vyao, dini zao, kabila zao katika kuhakikisha kuwa wanatetea 
vyema wananchi wao na wanasimamia vyema watendaji wa Halmashauri zao kwa
 ajili ya kuwaletea wananchi maisha bora.
Naye
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Leopold Chundu Ulaya alisema kuwa 
mafunzo walipatiwa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa 
Hombolo na TAMISEMI yatawasaidia kuhakikisha kuwa miradi yote inatekezwa
 kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Alisema
 kuwa watajitahidi kuunganisha nguvu kwa pamoja kwa kubadilika ili 
kuhakikisha kuwa wanatatua matatizo ya wananchi waliowachagua na 
kuwaletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Mkuu
 wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amesema kuwa atawachukulia hatua 
ikiwemo kuwapeleka katika Mamlaka zao za uteuzi viongozi na Madiwani 
ambao wamekuwa wakijitokeza kuwatetea watumishi waliosimamishwa au 
kufukuzwa kwa  makosa mbalimbali kama vile ubadhirifu wa mali za umma .
Bw.
 Mwanri alitoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya 
Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora yaliyofanyika wilayani Nzega
  kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi jamii ya fursa na 
vikwazo kwa maendeleo (O&OD) iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za 
miradi ya maendeleo (LGDG)
Alisema
 kuwa imekuwa ikijitokeza katika baadhi ya maeneo mtumishi anakuwa 
ametuhumiwa kwa makosa mbalimbali na kusimamishwa ili kupisha uchunguzi 
tuhuma zake kunajitokeza baadhi ya  madiwani au viongozi kujifanya wao 
ni watetezi wake bila  kujali hasara iliyotokana na utendaji wake na 
utovu wa nidhamu.
Bw.
 Mwanri alisema hali hiyo imekuwa ikijitokeza katika baadhi ya 
Halmashauri kwa sababu ya baadhi ya Madiwani au viongozi fulani kuwa na 
maslahi binafsi na mtuhumiwa kwa sababu wanaona kuwa kutokuwepo kwake ni
 pigo kwao.
Alisisitiza
 kuwa somo la wajibu na maadili walilofundishwa linawataka kuhakikisha 
kuwa wanakuwa wazalendo kwa kulinda maslahi ya wananchi na sio kikundi 
fulani cha waharifu au wezi.
“Nikimsikia
 mtu anamtetea mtumishi aliyefukuzwa au kusimamishwa kwa utovu wa 
nidhamu naanza nay eye kama yuko katika uwezo wangu nitamdoa  na yeye 
ili akamtetee vizuri akiwa nje  …na kama ni Diwani nitampeleka katika 
Chama chake kwa kuwa ndio kilichompa dhamana ya kwenda kwa wananchi 
kuomba kura ili aweze kuchukuliwa hatua kwa sababu ya kuwasaliti 
wananchi waliomchagua” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aliwataka
 Madiwani wawe na uchungu na wananchi kwanza na kuacha kutetea maovu 
katika Halmashauri zao kama wanahitaji maendeleo ya watu wao yaonekana 
na  majina yao yawekwe kwenye Historia nzuri na sio ile ya kudharauliwa 
hata na vijana wadogo.
Naye
 Afisa Utumishi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI Debora Mkemwa akitoa mada 
kuhusu nidhamu kwa watumishi na mashauri ya nidhamu kwa Watumishi wa 
Serikali za Mitaa alisema kuwa uchunguzi wa awali unafanyika kabla ya 
hatua za kinadhamu kwa mtumishi  hazijachukuliwa ili kujiridhisha iwapo 
zipo sababu za msingi za kuanzishwa mchakato huo.
 
 
 
0 comments:
Post a Comment