Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Friday, June 9, 2017

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA TANO BARANI AFRIKA KWA WINGI WA WATU.

TANZANIA ni nchi ya tano katika Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, na serikali imesema idadi hiyo na kasi ya ongezeko imekuwa changamoto kubwa katika harakati za kupunguza umasikini na kuimarisha utoaji wa huduma.

Aidha, ni nchi ya pili kwa ustawi wa maisha ya wananchi katika Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema Tanzania ina wastani wa ongezeko la watu la asilimia 2.7 kwa mwaka, na hadi kufikia mwaka 2016, ilikadiriwa kuwa na watu 48,076,698.

“Kwa makadirio haya, Tanzania inakuwa ni nchi ya tano kwa idadi kubwa ya watu Barani Afrika, ikitanguliwa na nchi nne ambazo ni Nigeria, Ethiopia, Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).”

Dk Mpango akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Mwaka 2017/18, alisema idadi kubwa ya watu na kasi ya ongezeko imekuwa ni changamoto kubwa katika harakati za kupunguza umasikini na kuimarisha utoaji wa huduma.

“Kwa kuzingatia hali hii, serikali imeendelea kuongeza na kuboresha upatikanaji wa elimu ya msingi hususan kwa wasichana,” alieleza Dk Mpango na kuongeza: “Kwa upande mwingine, idadi kubwa ya watu ni fursa pia kwa maana ya soko la bidhaa na huduma, ikiwa itaendana na maendeleo ya stadi, teknolojia, ujasiriamali na pato la kila mwananchi.”

Alieleza kuwa licha ya hatua hizo, bado kumekuwa na changamoto nyingine kutokana na kasi kubwa ya uhamiaji mijini, ambapo sasa takriban asilimia 30 ya watu nchini wanaishi mijini.

Alisema kasi hiyo ya mabadiliko ya idadi ya watu na uhamiaji mijini inadunisha kasi ya kuboresha upatikanaji wa nyumba na makazi yaliyopangwa na pia utoaji wa huduma zinazoendana na idadi ya wakazi mijini.

Kwa upande wa ustawi wa jamii, alieleza kuwa maisha ya watu yameendelea kuboreka kama inavyothibitishwa na taarifa ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Watu mwaka mwaka 2016.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa kigezo cha fahirisi ya maendeleo ya watu (HDI) ustawi wa Watanzania umeendelea kuimarika kutoka alama 0.521 mwaka 2014 hadi alama 0.531 mwaka 2015.

“Kigezo hiki huzingatia viashiria kadhaa vya maendeleo na ustawi hususan, muda wa kuishi baada ya kuzaliwa, elimu na wastani wa kipato cha mwananchi. “Kwa kutumia kigezo hiki, Tanzania ni nchi ya pili kwa ustawi wa maisha ya wananchi katika Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya iliyofikia alama 0.555 katika kipindi hiki,” alifafanua Dk Mpango.

Alisema matokeo ya Tanzania ni matokeo ya jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji safi na salama, na umeme katika maeneo ya vijijini na mijini.

Alitoa mfano idadi ya wananchi waliofikiwa na huduma ya umeme hadi Machi 2017 ilifikia asilimia 67.5 ikilinganishwa na asilimia 40 iliyofikiwa Aprili, 2016. Alisema kwa maeneo ya mijini, idadi ya wananchi wanaopata umeme ilifikia asilimia 97.3 Machi 2017 ikilinganishwa na asilimia 63.4 mwaka 2014/15, na upande wa maeneo ya vijijini ilifikia asilimia 49.5 Machi 2017 ikilinganishwa na asilimia 21.0 mwaka 2014/15.

“Kwa upande wa upatikanaji wa maji, idadi iliongezeka kutoka watu 21,900,000 Juni 2016 hadi 22,951,371 Machi 2017. “Kumekuwa na mafanikio pia kwa upande wa elimu, ambapo uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka milioni 1.5 mwaka 2014 hadi milioni 2.1 mwaka 2016,” alieleza.

Vile vile alisema idadi ya wananchi wanaonufaika na huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imeongezeka kutoka 3,377,023 mwaka 2015/16 hadi 3,880,088 Machi 2017.

Aidha, alisema wanufaika wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wameongezeka kutoka 8,717,130 mwaka 2015/16 hadi kufikia wanufaika 9,573,906 Machi 2017.

 Alifafanua kuwa pamoja na kupunguza umasikini wa mahitaji ya msingi, ni dhamira ya serikali kuhakikisha kuwa idadi ya Watanzania wanaokosa mlo kwa siku au kuishi kwa mlo mmoja inapungua kutoka kiwango cha asilimia 9.7 kwa sasa kufikia asilimia 5.7 na 4.4 ifikapo mwaka 2020 na 2025, kwa mtiririko huo.

Alizitaja hatua zinazochukuliwa kufikia lengo hilo ni kuimarisha uzalishaji na hivyo upatikanaji wa chakula katika kaya; kuongeza fursa za ajira mijini na vijijini

0 comments:

Post a Comment