Kwa uchache watu 14 wameuawa kusini magharibi
mwa Somalia wengi wao wakiwa ni raia baada ya kuzuka mapigano baina ya
wanajeshi wakigombea chakula cha misaada
Mapigano hayo yalizuka baada ya baadhi ya wanajeshi kujaribu kuiba chakula cha misaada ambapo kundi jingine la wanajeshi lilikuja na kuwazuia wenzao hao.
Mohammed Ahmed mmoja wa maafisa katika hospitali kuu ya Baidoa amewaambia waandishi wa habari kwamba, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo hali zao ni mbaya, inagawa wanaendelea kupata matibabu.
Mbali na majanga hayo ya kimaumbile, Somalia inakabiliwa pia na harakati za kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, nusu ya raia wa Somalia ambao ni karibu watu milioni sita na laki mbili wanahitajia msaada wa haraka huku watoto laki tatu na elfu 63 wakikabiliwa na hali mbaya sana ya utapiamlo.
0 comments:
Post a Comment