Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Monday, August 21, 2017

NEC YATEUA MADIWANI WAPYA 12 WA VITI MAALUM.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
UTEUZI WA MADIWANI WANAWAKE WA VITI MAALUM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa Mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika leo tarehe 21 Agosti, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa imewateua Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kumi na wawili (12) kujaza nafasi wazi za Madiwani katika Halmashauri mbalimbali Tanzania Bara.
Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu walioteuliwa ni kama ifuatavyo: NA. JINA CHAMA HALMASHAURI 1. 1 Ndugu Saida Idrisa Kiliula CUF Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa 2. Ndugu Sophia Charokiwa Msangi CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga 3. Ndugu Shahara Selemani Nduvaruva CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali 4. Ndugu Neema K. Nyangalilo CCM Halmashauri ya Manispaa ya Ilal
10. Ndugu Ikunda Massawe CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Hai
5. Ndugu Farida Zaharani Mohamed CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero 6. Ndugu Lucia Silanda Kadimu CCM Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) 7. Ndugu Amina Ramshi Mbaira CCM Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu 8. Ndugu Janeth John Kaaya CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Meru 9. Ndugu Sara Abdallah Katanga CHADEMA Halmashauri ya Manispaa ya Ilala 11. Ndugu Tumaini Wilson Masaki CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Siha
12. Ndugu Elizaberth Andrea Bayyo CHADEMA Halmashauri ya Mji wa Mbulu
Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi. Imetolewa leo tarehe 21 Agosti, 2017

Kailima, R. K

0 comments:

Post a Comment