Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Monday, August 21, 2017

Tanzania yatishia kufuta usajili kwa waendeshaji utalii wasio waaminifu.

Serikali ya Tanzania imetishia kufuta usajili kwa kampuni za kusafirisha watalii zinaozokwenda kinyume na sheria na kanuni za sekta ya utalii za Tanzania.
Onyo hilo limetolewa na waziri ya Maliasili na Utalii wa Tanzania Prof Jumanne Maghembe kwa watu wasiofuata maadili, na wanaowahadaa watalii wanaotaka kwenda kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.
Prof Maghembe amemuagiza mkurugenzi wa idara ya utalii, Bw Deograsias Mdamu kuwabaini watu wa aina hiyo. Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua kali na nyepesi dhidi ya watu hao kwa manufaa ya sekta ya utalii.

0 comments:

Post a Comment