Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Sudan Kusini, Bw. David Shearer jana amesema mchakato wa amani ya Sudan Kusini unaoendelezwa polepole.
Akiliarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya sasa ya Sudan Kusini, Bw. Shearer ambaye pia ni kiongozi wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo, amesema, pande mbalimbali zinazopingana nchini Sudan Kusini hazina nia ya dhati ya kufanya mazungumzo.
Vilevile amesema watu milioni 7.6 nchini Sudan Kusini wanahitaji msaada wa kibinadamu ambao kama ukikosekana, maisha ya watu wengi wa nchi hiyo yatakabiliwa na tishio. @CRI
0 comments:
Post a Comment