UONGOZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),
umetekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufungua ofi si zake nchini
Rwanda kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa nchi hiyo.
TPA imeshakamilisha taratibu zote na tayari ina ofisi na mtumishi wake nchini humo, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo jijini Kigali. Aidha, imeelezwa kuwa kumekuwa na ongezeko la shehena ya mizigo ya Rwanda kwa wastani wa asilimia 9.9 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano, kutoka tani 630,000 mwaka 2012/2013 mpaka tani 950,000 mwaka 2016/2017.
Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko hivi karibuni alipokutana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura aliyeitembelea mamlaka hiyo. “Ufunguzi wa ofisi hiyo utasaidia sana kuimarisha huduma kwa wateja wetu wa Rwanda ambao wanatumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Kakoko.
Aidha, alisema wametoa upendeleo Rwanda kwa kuipatia eneo maalumu la kuhifadhia mizigo iendayo nchini humo. Inajenga bandari kavu katika maeneo ya Kwala na Ruvu, mkoani Pwani, hali itakayorahisha usafirishaji wa mizigo badala ya kuwafanya wafanyabiashara kufuata mizigo hadi Dar es Salaam.
Hatua hiyo imepongezwa na Balozi Kayihura, akisema anaushukuru uongozi wa TPA na Serikali ya Tanzania kwa kuwajali watu wa Rwanda. Balozi Kayihura aliongeza kuwa biashara kati ya Tanzania na Rwanda imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni baada ya TPA kuimarisha huduma zake.
“Kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikihudumia asimilia 90 ya mizigo yote inayoingia na kutoka Rwanda, hivyo kuweka rekodi ya ukuaji wa haraka sana wa mizigo ya Rwanda inayohudumiwa nchini Tanzania,” alisema Balozi Kayihura.
Mbali ya kuwa mbioni kufungua ofisi nchini Rwanda, TPA ilishiriki pia Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Rwanda hivi karibuni huku ikilenga kuwa karibu na wateja wake na ilifanikiwa kukutana na wafanyabiashara walioelezea kuridhishwa na huduma za bandari hiyo, huku wakiahidi kuitumia zaidi na zaidi katika kupitisha mizigo yao.
RAIS MAGUFULI
Akizungumzia huduma za bandari katika kukuza uchumi wa nchi, mwaka jana Rais Magufuli alisema yeye na Rais Paul Kagame wa Rwanda wamekubaliana kufungua ofisi ya TPA jijini Kigali ili kuondoa usumbufu kwa wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam.
“Tumeamua TPA ifungue ofisi Kigali nchini Rwanda ili wafanyabiashara badala ya kuwa wanakuja na nyaraka Dar es Salaam na kuongeza gharama sasa watakuwa wanaanzia Kigali,” alisema.
UPANUZI BANDARI
Julai mwaka huu, Rais Magufuli aliweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam unaotarajiwa kugharimu Sh bilioni 922 ili kuifanya kuwa ya kisasa itakayoweza kupokea meli na shehena kubwa za mizigo kwa wakati mmoja.
“Mradi huu utakapokamilika utainufaisha Taifa letu na nchi jirani kama vile Malawi, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda, Uganda na Burundi ambazo zinategemea bandari yetu kusafirisha mizigo,” alisema na kuongeza kuwa, bandari hiyo ni lango kuu la biashara na ni kitovu cha uchumi wa nchi, hivyo kama itaboreshwa ufanisi na uwezo wake itasaidia kukuza uchumi.
Aidha, alisema uboreshaji wa bandari hiyo utaondoa ucheleweshaji wa upakuaji na upakiaji wa mizigo uliokuwa ukisababishwa na ufinyu wa gati. “Mradi huu ukikamilika utaifanya badari ya Dar es Saalam kuwa ya mfano na kutakuwa hakuna ucheleweshaji wa mizigo na itachangia maendeleo kiuchumi siyo tu kwa Tanzania bali hata kwa zile nchi zitakazokuwa zinatumia bandari hii kupitisha mizigo yao,” alisema.
Aidha, aliitaka TPA kuimarisha ulinzi katika bandari hiyo ili kuifanya kuwa mahali salama pa kupitishia mizigo na kuhakikisha mizigo yote inayopita bandarini taarifa zake zinajulikana.
Naye Kakoko alisema uboreshaji wa bandari hiyo utaiwezesha kuhudumia shehena ya mizigo kutoka tani milioni 14 zinazohudumiwa kwa sasa hadi kufikia tani milioni 28 ifikapo mwaka 2022 na pia itaweza kuhudumia meli kubwa zenye urefu wa hadi meta 320.
Katika uboreshaji wa bandari hiyo, Serikali ya Tanzania inachangia dola milioni 63.4, Benki ya Dunia dola milioni 345.2 na Serikali ya Uingereza dola milioni 12.4. Mradi unategemewa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 36 chini ya kampuni ya China Harbour Engineering.
VIFAA VYAWASILI
Wiki iliyopita, TPA ilipokea meli tano, tatu kati ya hizo zikiwa na vifaa vya ujenzi wa gati maalumu la magari na uboreshaji wa gati namba 1 -7 na mbili zitakazotumika kuchimba kwa lengo la kuongeza kina cha bandari kuanzia katikati ya mwezi huu.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Fred Liundi amethibtisha kuwasili kwa vifaa hivyo utakaoruhusu kuanza kwa ujenzi huo wa mradi ujulikanao kama ‘Dar es Salaam Maritime Gateway Project’.
RELI YA KISASA
Aidha, katika kutambua umuhimu wa Reli ya Kati kwa uchumi wa Tanzania na Rwanda, Tanzania imeanza kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge”. Naye Rais Kagame akiwa nchini mwaka jana, alimhakikishia Rais Magufuli kuwa serikali yake itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya nchi yake na Tanzania kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili

0 comments:
Post a Comment