
Maafisa wa polisi wanasema kuwa
mwanamume mmoja katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana amemuua
mkewe baada ya kukataa kushiriki naye tendo la ndoa.
Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliambia BBC.
Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
''Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata'', bwana Jaglan aliambia BBC.
Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja. Wana watoto wawili.
Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa
0 comments:
Post a Comment