Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
watoto UNICEF limesema licha ya hatua zilizopigwa kimataifa, mtoto 1
kati ya 12 duniani wanaishi katika nchi ambazo matarajio yao leo ni
mabaya kuliko ya wazazi wao.
Ripoti ya UNICEF imesema watoto milioni 180 wanaishi katika nchi 37 ambako wanakabiliwa na ufukara, kutosoma au kuuawa kikatili kuliko watoto walioishi katika nchi hizo hizo miaka 20 iliyopita.
Mkurugenzi wa takwimu, utafiti na sera wa UNICEF Laurence Chandy anasema wakati kizazi kilichopita kimeshuhudia hatua kubwa katika kupandisha kiwango cha maisha ya watoto duniani, ukweli unasalia kwamba watoto kutoka jamii za walio wachache zilizosahaulika wametengwa katika hatua hizo na sio kosa lao wala la familia zao.
UNICEF inasema sababu kubwa ni, vita, ugaidi, matatizo ya kiuchumi, kuongezeka kwa idadi ya watu na umasikini.
0 comments:
Post a Comment