Baada ya jeshi kuchukua udhibiti.
Vifaru vya jeshi la Zimbabwe vimezifunga njia kuelekea bungeni,
makao makuu ya chama tawala cha Zanu-PF na katika ofisi ambako kawaida
rais Robert Gabriel Mugabe hukutana na mawaziri wake. Masaa machache
kabla ya hapo, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kijeshi, Major jenerali
Sibusiso Moyo alitangaza kupitia televisheni ya nchi hiyo kwamba jeshi
limeingilia kati dhidi ya "wahalifu wanaomzunguka rais Mugabe, na
kukanusha njama yoyote ya mapinduzi."Tungependa kulihakikishia taifa
kwamba mheshimiwa, rais wa jamhuri ya Zimbabwe, mkuu wa vikosi vya
wanajeshi wa Zimbabwe, komredi Robert Gabriel Mugabe na familia yake
wako salama usalimina."
Wapi Mugabe amewekwa haijulikani.
Major jenerali Sibusiso Moyo amesema lengo la kuingilia kati ni kuwaandama "wahalifu wanaomzunguka Mugabe". Haijulikani lakini wapi Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 na mkewe wamewekwa. Inaonyesha kana kwamba wanashikiliwa jeshini.
Wanajeshi wote wametakiwa warejee kambini haraka na walioomba kikizo wamekataliwa. Miripuko mitatu imesikika jana usiku mjini Harare.
Opereshini hizo za jeshi zinadhihirika zimelenga kudhdibiti hali ya mambo nchini humo. Mkuu wa vikosi vya wanajeshi Constantino Chiwenga alitishia jumatatu iliyopita "wataingilia kati" kusitisha mivutano ya kisiasa nchini. Chama tawala cha Zanu-PF kilijibu kwa kumtuhumu jenerali huyo kufanya uhaini.
Jeshi lakini linasifiwa na wazee waliopigania ukombozi kwa "kukomesha bila ya kumwaga damu, mitindo ya kutumiwa vibaya madaraka."Wanajeshi watairejesha Zimbabwe katika mfumo halisi wa kidemokrasi" na kuigeuza nchi iwe ya kimambo leo.
SADC iko tayari kupatanisha.
Ubalozi wa Marekani umefungwa na raia wa Marekani wametakiwa kubakia majumbani mwao. Onyo kama hilo limetolewa pia na Uingereza.
Nae rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameelezea matumaini yake kwamba hakuna mageuzi ya kinyume na katiba yatakayotokea baada ya jeshi kudhibiti madaraka mjini Harare. Rais Zuma amewatolea wito serikali na jeshi wamalize tofauti zao kwa amani akiahidi jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika iko tayari kusaidia.
Hali ya wasi wasi imeenea huku wazimbabwe wakipiga foleni mbele ya benki zao kuchukua akiba wanazoruhusiwa kuchukua. Wengine, simu mkononi kujua yanayoendelea huku wakielekea madukani au kazini.
Jeshi nchini Zimbabwe linawashikilia rais Robert Mugabe
na mkewe na kuzilinda ofisi za serikali pamoja na kupiga doria katika
mitaa ya mji mkuu Harare.Hali ya wasi wasi imetanda mji mkuu Harare
Wapi Mugabe amewekwa haijulikani.
Major jenerali Sibusiso Moyo amesema lengo la kuingilia kati ni kuwaandama "wahalifu wanaomzunguka Mugabe". Haijulikani lakini wapi Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 na mkewe wamewekwa. Inaonyesha kana kwamba wanashikiliwa jeshini.
Wanajeshi wote wametakiwa warejee kambini haraka na walioomba kikizo wamekataliwa. Miripuko mitatu imesikika jana usiku mjini Harare.
Opereshini hizo za jeshi zinadhihirika zimelenga kudhdibiti hali ya mambo nchini humo. Mkuu wa vikosi vya wanajeshi Constantino Chiwenga alitishia jumatatu iliyopita "wataingilia kati" kusitisha mivutano ya kisiasa nchini. Chama tawala cha Zanu-PF kilijibu kwa kumtuhumu jenerali huyo kufanya uhaini.
Jeshi lakini linasifiwa na wazee waliopigania ukombozi kwa "kukomesha bila ya kumwaga damu, mitindo ya kutumiwa vibaya madaraka."Wanajeshi watairejesha Zimbabwe katika mfumo halisi wa kidemokrasi" na kuigeuza nchi iwe ya kimambo leo.
SADC iko tayari kupatanisha.
Ubalozi wa Marekani umefungwa na raia wa Marekani wametakiwa kubakia majumbani mwao. Onyo kama hilo limetolewa pia na Uingereza.
Nae rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameelezea matumaini yake kwamba hakuna mageuzi ya kinyume na katiba yatakayotokea baada ya jeshi kudhibiti madaraka mjini Harare. Rais Zuma amewatolea wito serikali na jeshi wamalize tofauti zao kwa amani akiahidi jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika iko tayari kusaidia.
Hali ya wasi wasi imeenea huku wazimbabwe wakipiga foleni mbele ya benki zao kuchukua akiba wanazoruhusiwa kuchukua. Wengine, simu mkononi kujua yanayoendelea huku wakielekea madukani au kazini.
0 comments:
Post a Comment