Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Wednesday, November 8, 2017

Maandamano ya kisiasa yaendelea nchini Togo

Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Togo Lome hapo jana wakishinikiza kujiuzulu rais wa nchi hiyo Faure Gnassingbe ambaye familia yake imeliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi kwa zaidi ya miaka 50.

Maandamano hayo yamefanyika baada ya waziri anayehusika na masualaya utalii nchini humo Yaovi Attigbe Ihou kusema serikali ya nchi hiyo itachukua hatua zote za lazima kuanzisha mazungumo na kada ya kisiasa nchini humo huku mwanasiasa mkongwe wa upinzani Jean-Pierre Fabre akisema wao pia wanaunga mkono majadiliano hayo lakini wangependelea zaidi kujadili juu ya kuachia madaraka kwa Faure Gnassingbe.
Takribani watu 16 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa tangu maandamano ya kwanza yalipofanyika mwishoni mwa mwezi August.

0 comments:

Post a Comment