
Kesi mbili zimewasilishwa katika mahakama ya juu nchini Kenya, zikitaka kufutwa kwa ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kufuatia uchaguzi wa tarehe 26 mwezi Oktoba.
Kesi hizo ziliwasilisha mahakamani Jumatatu saa chache kabala ya siku ya mwisho.
Aliyekuwa mbunge wa kilome Harun Mwau na mawakili Njonjo Mue na Khelef Khalifa, wanasema kuwa katiba ilikiukwa wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.
Kesi ya mwau ambayo inawashtaki IEBC, mwenyekiti wake na Rais Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba, inasema kuwa kushindwa kwa IEBC kuruhusu vyama kuandaa uchaguzi wa vyama, kuliwanyima wale ambao walitaka kugombea fursa ya kufaya hivyo.
Mwau alijumuisha kipengee cha uamuzi wa mahakama, kuwa mgombea kwa chama cha United Democratic Cyrus Jirongo alikuwa amefilisika kwa hivyo hakustahili kuwania urais.
Ndubi aliwaambia waandishi wa habari kuwa kumjumuisha Odinga kwenye makaratasi ya kura licha ya yeye kujiondoa kuliwachanganya wapiga kura.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais baada ya marudi ya uchaguzi ulioandaliwa tarehe 26 mwezi Agosti akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati alisema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.
0 comments:
Post a Comment