Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Wednesday, November 8, 2017

Maofisa wa usalama wa Kenya wafanya opresheni ya kuwakamata wapiganaji wa Kundi la Al-Shabaab

Maofisa wa usalama wa Kenya wameanza opresheni ya kuwakamata wapiganaji wa Kundi la Al-Shabaab, walioshambulia na kuteketeza magari mawili ya polisi yaliyokuwa yanasindikiza basi la abiria Jumatatu katika kaunti ya Mandera, kaskazini mwa Kenya.

Naibu mkuu wa kaunti ya Mandera Kusini Bw Daniel Bundotich amesema wapiganaji hao waliyafyatulia risasi magari hayo ya polisi yanayokuwa yanalinda basi la abiria lililokuwa linaelekea Mandera kutoka Nairobi. 

Shambulizi hilo lilitokea eneo la Dabacity la kaunti ya Mandera, lililoko kwenye mpaka kati ya Kenya na Somalia, lakini hakuna yeyote anayejeruhiwa.

Mkuu wa Kaunti ya Mandera Bw Fredrick Shisia amesema viongozi wa usalama wameweka mpango maalumu dhidi ya washambuliaji hao.

0 comments:

Post a Comment