Wanafunzi 6 wa shule ya msingi
Kihinga mkoani Kagera kusini magharibi mwa Tanzania wamefariki dunia na
wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Augustine Orom huo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Kwa mujibu wa Dokta Sista Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea
0 comments:
Post a Comment