Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Wednesday, November 1, 2017

MIUNDOMBINU UWANJA WA NDEGE WA JNIA NI KIKWAZO KWA WALEMAVU.

Miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere umetajwa kuwa kikwazo kwa watu wenye ulemavu pale wanapohitaji huduma mbalimbali.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Ajira, Bunge, Vijana na wenye ulemavu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye ulemavu, Stellah Ikupa Alex amesema hayo baada ya kutembelea na kuona miundombinu ya uwanja huo.

“Suala la miundmbinu bado ni changamoto katika maeneo mengi katika viwanja vya ndege, kwahiyo nitoe rai kwa wajenzi wote kwa wa haya majengo ambayo ni public lakini sio tu public hata nyumbani kwa mfano unajenga nyumba yako ambayo ina ngazi moja, mbili, tatu, nne sasa unapata mgeni ambaye ana wheel chair anapandaje zile ngazi,” alihoji Stellah.

“Kwahiyo niseme suala la miundo mbinu lizingatiwe maeneo yote hilo ni ombi langu kwa Watanzania wote lakini katika ya pia haya maeneo ambayo ni public tukizingatia miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu.”

Nao baadhi ya wafanyakazi wa uwanja wa Taifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere wameahidi kushughulikia changamoto za abiria wenye ulemavu

0 comments:

Post a Comment