Mkataba mpya wa kimataifa wa kulinda haki za waandishi wa habari umetiwa saini huko Tunisia.
Anthony Bellanger Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la
Waandishi wa Habari (IFJ) amesema huko Tunisia kuwa mktaba huo mpya
umesainiwa kwa lengo la kuunda kamati itakayokuwa na jukumu la kudhamini
usalama na kulinda maisha ya waandishi wa habari.
Bellanger ameongeza kuwa kamati hiyo
itakayoundwa itakuwa na wajumbe 15 na wanachama wake watachaguliwa
kutoka nchi zilizosaini kipengee cha 19 cha azimio la kimataifa la haki
za kiraia na kisiasa ambacho kinabainisha wazi suala la kulindwa haki ya
uhuru wa kifikra na kujieleza.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa
la Waandishi wa Habari (IFJ) amesema kuwa vitendo vya utumiaji mabavu
dhidi ya waandishi wa habari duniani vinaongezeka kila uchao na uhalifu
mwingi unaowakumba wana taaluma hao haufatiliwi na wahusika wa vitendo
hivyo hawachukuliwi hatua za kisheria au kuadhibiwa.
Ni kwa sababu hiyo ndio maana Mkutano wa
Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari umeratibu mpango mpya
kwa ajili ya kuuungwa mkono kimataifa waandishi wa habari sambamba na
kulindwa maisha yao wakati wa vita na amani ambao utawasilishwa katika
kikao cha kawaida cha Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment