Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Sunday, November 26, 2017

Rais Magufuli awapa siku saba vigogo sita wakiwemo mawaziri wake wawili

ca1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
ca2 
  Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa Mamlaka ya Mapato( TRA),  Mamlaka ya Bandari(TPA), Takukuru na Wizara ya Fedha kuhakikisha inatoa taarifa ni nani alihusika kuagiza magari 50 kupitia mgongo wa Ofisi ya Rais.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo Jumapili Novemba 26 baada ya kufanya ziara ya ghafla bandarini mara baada ya kutembelea meli ya Wachina iliyofanya matibabu kwa Watanzania kwa muda wa siku 5.
Magari hayo aina ya ambulance ambayo mpaka leo yapo bandarini, yaliagizwa mwaka 2015 kupitia majina ambayo hayatambuliki na Ofisi ya Rais.
Kabla ya kutoa maagizo hayo, Rais amewahoji IGP, Waziri wa Fedha, Kamishna Mkuu wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ambao hata hivyo hawakuwa na mujibu kuhusu nani hasa mwagizaji wa magari hayo.
"Natoa onyo kwa mawaziri na wateule wale wote waliotangaza, sitaki mpaka nije kubaini uozo mimi mwenyewe ninataka mpigane kuhakikisha uozo wote unaondoka, safari nyingine nikigundua jambo lolote na wewe ni eneo lako hautapona," amesema.
Ameongeza,  "Ninatoa siku saba,  nataka aliyeagiza haya magari kwa mgongo wa Ofisi ya Rais atambulike ni nani na ninatoa maagizo hata kama ni mtu mkubwa kiasi gani atambulike nahitaji mujibu."
Wakati huohuo Rais Magufuli ametembea umbali wa zaidi ya mita 700 ili kukagua magari ya polisi ambayo yaliingizwa nchini mwaka 2015 lakini bado zaidi ya magari 50 yameendelea kubaki eneo la bandari.
Amemwagiza IGP kuhakikisha anayakagua magari hayo na kuyatoa bandarini ili yakafanye kazi ambayo ilikusudiwa.
  "Kwa nini magari yanakuja hapa yanakaa miaka 10, wakati sheria inasema ni siku 21? Amehoji Rais Magufuli.

 ca3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo toka viongozi wa Mamlaka ya Bandari, Jeshi la Polisi na TRA kuhusiana na magari ya wagonjwa 53 yaliyofichwa katika kona moja ya Bandari ya Dar es salaam huku wamiliki wake wakiwa hawajulikani alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
ca4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua sehemu ya magari zaidi ya 6000 yaliyopo bandari ya Dar es salaam mengine yakiwa hapo kwa miaka zaidi ya kumi bila kuchukuliwa na wenye nayo alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
ca5

ca6 ca7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo kuhusu magari zaidi ya 50 ya Jeshi la Polisi yaliyopo bandarini toka mwaka 2015 kwa sababu ya kutolipiwa  ushuru alipofanya ziara ya kushtukiza leo Jumapili Novemba 26, 2017
ca8

PICHA NA IKULU

0 comments:

Post a Comment