Diwani wa kata ya
Kiwangwa Malota Kwaga,akitoa taarifa ya kata kwenye kikao cha baraza la
madiwani la halmashauri ya Chalinze .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya
madiwani,watendaji na wakuu Wa Idara katika halmashauri ya Chalinze
mkoani Pwani ,wakisikiliza taarifa kutoka kwa diwani wa kata ya Kiwangwa
Malota Kwaga,wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya ardhi maliasili Chalinze
Zaina Kijazi.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
WIMBI la tembo
limeibuka na kuharibu mazao ya wakulima wa baadhi ya vijiji vya kata ya
Kiwangwa ,Mkange na Kibindu vinavyozunguka hifadhi ya Taifa ya Saadan na
vilivyo karibu na Mto Wami .
Aidha watu watatu wanadaiwa kuuawa kutokana na wanyamapori wakiwemo tembo na fisi.
Kati ya watu hao
wawili wamefariki baada ya kujeruhiwa na fisi katika kijiji cha Kiwangwa
na mtu mwingine alikufa kutokana na kujeruhiwa na tembo huko kwa
Kwamduma.
Akitoa taarifa hiyo
kwenye kikao cha madiwani cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ngazi
ya kata kipindi cha robo mwaka ,diwani wa kata ya Kiwangwa Malota Kwaga
,alisema tembo wamekuwa tatizo na kutishia maisha ya watu .
Alieleza mazao yaliyoliwa zaidi ni matikitimaji ,mapapayi,mahindi,migomba na nyanya.
Kwaga alisema ,zipo hatua alizozichukua ambazo ni kupeleka taarifa halmashauri na wilaya idara ya ardhi maliasili na utalii.
“Idara husika ilisema ipo sheria ya kulipa kifuta jasho walioathiriwa ama kuuawa na wanyamapori “
“Kwa upande wangu
kauli hii hainifurahishi na haina mashiko kwani wakulima wameshapata
hasara lakini badala ya kulipwa fidia wanaambiwa wanalipwa kifuta jasho”
alieleza Kwaga.
Kwaga alisema pia
hifadhi ya Taifa -TANAPA na baadhi ya viongozi wa halmashauri walikwenda
kuzungumza na wananchi juu ya tatizo hilo na kutoa elimu .
Alisema kwasasa
wakulima walioliwa mazao yao wameshaorodheshwa majina yao na watakwenda
kufanyiwa uhakiki kwa ajili ya kulipwa fedha hizo .
Nae mkuu wa idara ya
ardhi na maliasili katika halmashauri ya Chalinze ,Zaina Kijazi alikiri
kuwepo kwa tatizo la wanyamapori tembo na kiboko kula mazao ya
wakulima.
Alisema tembo
wameharibu mazao hekari zaidi ya 200 ,kifo cha mtu mmoja
kilichosababishwa na tembo na vifo viwili vilivyotoka na fisi.
Zaina alisema tembo
wanangia kwenye maeneo ya wakulima ni kutokana na kukariri njia ya
mapito yao kutoka Saadan wakielekea Wamimbiki na Mikumi .
Tembo ni wanyama
wanaopenda kula maboga,miwa na matikitimaji hivyo ni changamoto kwani
ndio mazao yanayolimwa zaidi na wakulima hao.
Kwa upande wake
mkulima wa kijiji cha Matipwili Deus Mabirika alieleza ,mazao yake
yameharibiwa katika hekari moja ambapo miche ya mipapayi 294 aliyoinunua
kila mche 5,000 imeharibiwa yenye gharama ya mil.1.470.
Alisema kati ya hasara aliyoipata ameambiwa atapatiwa kifuta jasho 50,000 kiasi ambacho ni kidogo .
Mabirika aliiomba wizara ya maliasili kuangalia suala hilo kwani fedha hizo ni ndogo hazikidhi mahitaji.
0 comments:
Post a Comment