Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) litatoa mafunzo ya soka la ufukweni (Beach Soccer) kwa
vyuo mbalimbali hapa nchini vilivyothibitisha kushiriki Ligi Maalumu ya
soka la Ufukweni itakayoanza Novemba 18, 2017.
Kwa upande wa mafunzo ni kwamba
yatafanyia siku tano kabla ya kuanza kwa ligi hiyo ambako itakuwa ni
Novemba 13, mwaka hu. TFF imepanga kutoa mafunzo hayo kwa vyuo hivyo ili
wauelewe zaidi mchezo huo pamoja na sheria zake.
Tumepeleka mchezo huo kwenye vyuo ili
kutoa hamasa ya soka la ufukweni kuenea zaidi na kuweka hazina ya
wachezaji wa timu ya taifa.
Mpaka sasa vyuo 14 tayari vimethibitisha kimaandishi kushiriki kwenye mafunzo hayo.
Vyuo vilivyothibitisha kushiriki ni
Chuo cha Ardhi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo Cha Ufundi (DIT),
Chuo cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Elimu ya Tiba cha Kahiruki, Chuo
cha Elimu ya Biashara cha Lisbon, Chuo cha Silva , Chuo UAUT, TIA,
El-Maktoum collage Engineering, Magogoni, Chuo cha uandishi wa habari
DSJ na TSJ.
Mafunzo hayo yatatanguliwa na tukio la kukutana na viongozi wa vyuo shiriki hapo Novemba 10, 2017.
Wakati huo huo kozi ya waamuzi wa Soka
la Soka la Ufukweni imeanza leo Novemba 7, 2017 katika Makao Makuu ya
TFF Karume, Dar es Salaam ambayo yanatarajiwa kumalizika Novemba 12,
2017.

0 comments:
Post a Comment