Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Monday, November 6, 2017

UCHAGUZI KWA KONGO DRC KUFANYIKA 2018 BADALA YA 2019

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza disemba 23 mwaka ujao kuwa ndio siku ya uchaguzi mkuu utakaojumuisha wa rais, wabunge na viongozi wa serikali za majimbo badala ya kufanyika  mwaka 2019 kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali na Tume hiyo.

Kulingana na Chapisho hilo la ratiba ya Uchaguzi  matokeo ya muda yatatangazwa katika kipindi cha wiki moja baada ya upigaji kura kufanyika, mnamo tarehe 30 Desemba, lakini matokeo kamili yatatangazwa tarehe 9 januari, 2019 na siku tatu baadae Rais Mteule Kuapishwa kushika hatamu.

Licha ya kurejesha Nyuma tarehe ya Uchaguzi Upinzani Nchini humo umeendelea kushikilia Msimamo wake wa kutaka Kiongozi wa Taifa Hilo Joseph Kabila kuondoka mamlakani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.joseph kabila

0 comments:

Post a Comment