Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Thursday, March 8, 2018

DAWA 14 ZINAZOWEZA KUTIBU MAUMIVU YA GOTI

Gout au maumivu ya jongo kwa Kiswahili ni aina mojawapo ya maumivu ya mishipa na yanaweza kuleta maumivu makubwa katika maungio hasa katika kidole gumba cha mguu. Ishara kubwa za maumivu ya jongo ni maumivu ya uvimbe nyakati za usiku, kupatwa na hasira, na maumivu katika kidole kikubwa cha mguu. Unaweza pia kujisikia maumivu katika kifundo cha mguu, magotini au katika maungio mengine ya mwili.
Kitu kikubwa kinachosababisha maumivu ya jongo au gout ni kiasi kingi cha asidi katika mzunguko wa damu. Ikiwa unasikia maumivu kila mara katika mikono, vidole, magoti, katika maungio mbalimbali mwilini unashauriwa ukapate vipimo dhidi ya jongo.
Ukiacha maji ya kunywa ambayo ni mhimu sana katika kupunguza kiasi cha asidi mwilini, Hapa nimekuandikia mimea na matunda mhimu ambavyo vimejaribiwa na kuonyesha uwezo mkubwa katika kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

1.  Juisi ya limau

Juisi ya Limau ina viinilishe vya asili ambavyo vinaweza kusaidia kutibu maumivu ya jongo au gout kama tulivyozoea wengi wetu. Tafiti zinaonyesha kuwa matunda jamii ya chungwa kama vile machungwa yenyewe, machenza, na limau au ndimu husaidia kuyeyusha asidi iliyogandamana katika damu na hivyo kukupatia nafuu ya haraka itokanayo na maumivu ya gout. Tengeneza juisi hii ya limau ukichanganya na maji na unywe mara tatu kwa siku kwa majuma kadhaa.

2. Siki ya tufaha

Kwakuwa tunda la tufaha ni zuri katika kudhibiti gout hakuna shaka kwamba siki yake isiweze kudhibiti gout. Na kwa kawaida siki ya tufaha inafanya vizuri kutibu gout kuliko hata tunda lake. Siki ya tufaha ina asidi nzuri iitwayo acetic acid ambayo huongeza kiasi cha alkalini ndani ya mwili na kuunda usawa na mazingira mazuri ya pH (Potential Hydrogen) na hivyo moja kwa moja kuwa msaada mkubwa katika kupunguza na hata kutibu maumivu ya gout. Kumbuka pia hakuna utafiti ambao umefanywa kuthibitisha madai haya ya siki ya tufaha kuwa na uwezo huu. Unaweza kuchanganya siki ya tufaha katika chakula unachokula au kuongeza kijiko kikubwa kimoja katika glasi ya maji na unywe mara moja kila siku.

3. Baking Soda

Baking soda ina faida nyingi na matumizi mengi sana ikiwemo kukusaidia katika tatizo lako la gout. Sodium bicarbonate iliyomo kwenye baking soda huifanya damu kuwa na alkalini zaidi kitu ambacho ni mhimu katika kudhibiti gout. Chota kijiko kimoja kidogo cha baking soda na uiweke katika maji robo lita na unywe kutwa mara mbili kwa majuma kadhaa. Kama unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu usiitumie hii baking soda kujitibu gout.

4.  Nanasi

Nanasi lina kimeng’enya mhimu kiitwacho ‘bromelain’ ambacho kina sifa ya kuzuia muwako wa ndani ya mwili (inflammation). Kwahiyo kuwa na mazoea ya kula nanasi kila siku kunaweza kuzuia usipatwe au hata kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

5. Zabibu

Zabibu zina kiasi kingi cha kiuaji sumu na zinaweza kupunguza maumivu ya gout kwa haraka zaidi. Mbegu za tunda la zabibu zina kitu mhimu kiitwacho pycnogenolsambacho ni kiuaji sumu kingine kinachosaidia kupigana na aina zote za maumivu ya mishipa ikiwemo gout. Kula kila siku zabibu na utaona matokeo mazuri dhidi ya maumivu yako ya gout.

6. Tangawizi

Tangawizi ina matumizi mengi na imekuwa kwenye orodha ya dawa za asili au mbadala kwa ajili ya kutibu maradhi mengi kwa miaka mingi ikiwemo gout. Chemsha maji kama unachemsha maji ya chai, chukua tangawizi mbichi yaani ile ambayo siyo ya unga, kwangua (grate) kipande kimoja au viwili vya tangawizi ndani ya maji hayo yanayochemka, acha ichemke kama dakika 10, ipuwa na unywe kama chai kutwa mara tatu kwa wiki 3. Unaweza kuongeza asali au hata sukari kwenye huo mchanganyiko wa maji na tangawizi.

7. Ndizi

Ndizi zina kiasi kingi cha Potassiamu na Vitamini C na zinao uwezo pia wa kupunguza maumivu yatokanayo na gout kwa kuyeyusha asidi iliyoganda kwenye mkojo kuwa katika umajimaji ambao mwili wako unaweza kuutoa nje kirahisi. Kula ndizi kila mara kama unasumbuliwa na gout.

8. Mcheri

Tunda la mcheri lina kiasi kingi cha Vitamini C ambayo ni msaada mkubwa katika kupunguza asidi katika damu. Matunda 20 ya mcheri yakiliwa katika vipindi tofauti tofauti katika siku yanaweza kufanya maajabu dhidi ya maumivu yako ya gout. Ukinywa juisi ya mcheri pia ina matokeo yaliyo sawa na ukila matunda yake.

9. Unga wa mkaa

Pengine tayari unajuwa kuwa mkaa unao uwezo wa kuondoa harufu mbaya na hata sumu mwilini. Lakini lile ulikuwa hujuwi hadi sasa ni kuwa unga wa mkaa ambao unapatikana kwa kuusaga tu mkaa, unaweza pia kupunguza maumivu yatokanayo na gout.
Changanya unga huu wa mkaa katika maji, chukua kitambaa kilichotengenezwa kwa pamba na ukiloweke kwenye hayo maji kisha funika katika eneo lenye maumivu ukiacha hapo kwa dakika kadhaa mara kwa mara kwa siku kwa majuma kadhaa kutasaidia kama siyo kuondoa kabisa maumivu ya gout.

10. Maji ya Kunywa

Maji ni mhimu sana katika kushusha maumivu ya kwenye maungio ikiwemo gout. Maji ndicho kilainishi mhimu katika viungo vyote vya mwili. Kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10 za maji, maji yaliyo katika joto la kawaida na siyo ya baridi, ukifanya hivi kila siku baada ya wiki 2 au 3 utakuwa huru kabisa na maumivu ya gout.

11. Juisi ya maharage machanga (French Beans)

Kunywa Juisi hii ya maharage machanga kwa muda wa mwezi mmoja ili kupata matokeo mazuri. Shida itakuwa namna ya kuyapata haya maharage hasa kwa wale walio nje ya D’salaam lakini ukihitaji nijulishe.

12. Mharadali

Mharadali (Mustard) ni nzuri sana katika kupunguza maumivu ya gout. Chukuwa mharadali ya unga na uweke kwenye eneo lenye maumivu na uuache ufyonzwe na ngozi yako kwa usiku mzima na utakapoamka asubuhi utajisikia vizuri kabisa.

13. Mchanganyiko wa juisi ya matunda na mboga mboga
Mchanganyiko wa juisi ya tango, magimbi na karoti unawea kutumika kutuliza maumivu yatokanayo na gout haraka sana.

14. Mafuta ya nyonyo

Pasha kidogo mafuta ya nyonyo katika moto kisha pakaa eneo lenye maumivu taratibu kama vile unafanya masaji kwa dakika kadhaa mara mbili mpaka tatu kwa siku, fanya hivi kila siku mpaka utakapopona kabisa.

0 comments:

Post a Comment