Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Mpina ameamuru ng'ombe waliobaki hai kati ya 692 waliokufa katika Pori
la Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa wameshikiliwa warudishiwe kwa
wamiliki wa mifugo hiyo.
Waziri Mpina ameshangazwa kuona mizoga mingi kiasi hicho huku mifugo hai ikiishi zizi moja na iliyokufa, huku kukiwa na harufu mbaya
Imeelezwa kwamba mazingira hayo yamechangia kasi ya maambukizi ya magonjwa nyemelezi kuwa kubwa zaidi na kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo hiyo.
Hata hivyo baada ya kushudia Mizoga hiyo, Mh. Mpina amepokea taarifa ya Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji na wamiliki wa mifugo hiyo na kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao kukabidhiwa kwa wenyewe tangu Julai 27, mwaka jana.
Mifugo hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika hifadhi hiyo tangu mwezi machi mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment