Askofu wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani
tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini
siku zote tumekuwa nyuma.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima.
Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo.
"Hata kama tulisaini
mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu
makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari
kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa,
sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni
ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna
kwenda" alisema Gwajima
0 comments:
Post a Comment