Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Monday, May 15, 2017

"Nilijifanya kuwa mwanamume ili kufanya kazi katika mgodi Tanzania"

Pili Hussein
Pili Hussein alitamani kujiimarisha kimaisha na mawe ya thamani yanayosemekana kuwa nadra mara elfu mia moja kuliko almasi , lakini kwa kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia mavazi kama mwanamume na kuwadanganya wafanyikazi wenzake kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Pili alilelewa katika familia kubwa mjini Tanzania. Mtoto wa mchugaji ambaye aliyekuwa na mashamba makubwa, babake Pili alikuwa na wake sita na alikuwa miongoni mwa watoto 38.
Licha ya hayo yote alilelewa vyema kwa njia tofauti.
''Babangu alinichukulia kama mwanamume na nilikuwa nikichunga mifugo yake, lakini sikuyapenda maisha hayo kabisa'', alisema.
Hata ndoa yake haikuwa ya furaha, akiwa na umri wa miaka 31 Pili aliikimbia ndoa yake iliyokumbwa na migogoro ya kinyumbani.
Alipokuwa akitafuta ajira alijipata katika mji mdogo wa Mererani, Tanzania, uliopo chini ya mlima mkuu wa Kilimanjaro.
Eneo hilo ni nadra ulimwenguni kwa migodi kama ya violet - bluu inayoitwa tanzanite takes place.Mawe ya thamani ya tanzaniteMawe ya tanzanite yaliyopatikana mwaka 1967 na mchugaji wa kimaasai
''Sikwenda shule , kwa hivyo sikuwa na mambo mechi kuchagua,'' Pili alisema.
''Wanawake wahakuruhusiwa kwenye maeneo ya migodi hiyo, nikajitosa kama mwanamume shupavu na mwenye nguvu. Nilichukua suruali ndefu na kuzikata zikawa kama kaputula ili kufanana na mwanamume. Hivyo ndivyo nilivyofanya.''
Ili kukamilisha mabadiliko yake , alibadilisha pia jina lake.
''Niliitwa Uncle Hussein {akimaanisha mjomba Hussein}, sikumwambia yoyote kuhusiana na jina langu halisi la Pili.
Hata leo ukija katika kambi hiyo utanitafuta kwa jina hilo la Uncle Hussein.''
Kwenye migodi hiyo yenye joto ,uchafu mwingi na wenye kina cha mita mia moja chini ya ardhi Pili angefanya kazi kwa saa 10-12 kwa siku , akilima na kuchunga akiwa na matumaini ya kupata mawe hayo ya thamani kwenye mishipa ya mawe hayo ya grafiti.
''Ningeenda hadi mita 600 chini ya mgodi, mara kwa mara nikiwa shupavu kuliko wanaume wengine.
Nilikuwa na nguvu nyingi na niliweza kufanya kazi kama matarajio ya wanaume wengine wangefanya.''
Pili amesema hakuna aliyemshuku alikuwa mwanamke.
''Nilijifanya kama nyani aina ya Gorilla'' alisema, Nilipigana, lugha yangu ilikuwa mbaya , nilibeba kisu kikubwa kama Maasai.
Hakuna mtu alifahamu kwamba mimi ni mwanamke kwa sababu kile nilichokuwa nikifanya nilikifanya kama mwanamume.''
Baada ya mwaka mmoja, alipata utajiri , alipopata mawe mawili makubwa ya Tanzanite. Kutokana na pesa alizozipata alimjengea babake, mama na pacha wake nyumba mpya na akajinunulia vifaa zaidi na akaanza kuajiri wachimba migodi kumfanyia kazi.
Na kujificha kwake kuliwashawishi kwamba alichukua hatua zisizo za kawaida kwa utambulisho wake kujulikana.
Mwanamke mmoja aliripoti kwamba alikuwa amebakwa na wachimba migodi Pili akiwa miongoni mwa washukiwa.
''Polisi walipokuja, wanaume waliotekeleza ubakaji huo wakasema: 'Huyu ndio mwanamume aliyetekeleza hilo'' na nilipopelekwa katika kituo cha polisi , Pili akasema alikuwa hana namna bali kutoboa siri yake.''
''Aliwauliza polisi kumleta polisi mwanamke ili amchunguze kwamba yeye hakutekeleza kitendo hicho na baadaye aliachiliwa huru. Hata baada ya hilo wachimba migodi wenzake waliona vigumu kuamini walikuwa wamedanganyika kwa siku nyingi''
''Hawakuamini hata polisi waliposema kwamba alikuwa mwanamke'', alisema, ''haikuwa rahisi kwao kukubali hadi mwaka 2001 nilipoolewa na nikaanza familia.''
Kutafuta bwana wakati kila mtu amenizoea kama mwanamume haikuwa rahisi, Pili alipata bwana na akafanikiwa.
@bbcswahili Kwa kina bofya hapa

0 comments:

Post a Comment