Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Monday, May 15, 2017

SERIKALI KUTUNGA SHERIA YA SHISHA.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema serikali ina mpango mkakati wa kutengeneza utaratibu wa kudhibiti utumiaji, uuzwaji na usafirishwaji ya shisha nchini Tanzania ili kuweza kuokoa afya za Watanzania walio wengi.


Mwigulu Nchemba ameyazungumza hayo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge.

“Ni kweli serikali mara baada ya kuona kuwa matumizi ya shisha yanaleta athari kubwa kwa afya za binadamu kutokana na utafiti uliofanywa na wizara ya Afya serikali ina mpango mkakati wa kutengeneza utaratibu wa kudhibiti na kutungia sheria kupiga marufuku, utumiaji na uuzwaji na usafirishwaji nchini Tanzania ili kuweza kuokoa afya za Watanzania waliowengi ambao ni nguvu kazi ya Taifa letu,” alisema Mwigulu
Fuatilia kwa kina hapa chini mjadala juu ya shisha.

0 comments:

Post a Comment