Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Tuesday, August 22, 2017

Kenya na Tanzania zinapanga kufanya mazungumzo mwezi ujao ili kuondoa vizuizi vya kibiashara.



Rais Uhuru na Magufuli katika ikulu ya rais nchini Tanzania.

Katibu mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na ushirikiano ya Kenya Bw Chris Kiptoo amesema mazungumzo hayo yatakayofanyika nchini Tanzania ni mchakato unaofuata mazungumzo yaliyofanyika awali, ya kutatua hali ya kukwama kwenye biashara ya ngano na gesi. 

Amesema nchi hizo mbili zina nia ya kutafuta utatuzi wa kudumu wa migongano ya mara kwa mara ya kibiashara. 


Lengo la mazungumzo hayo ni kuhakikisha bidhaa za tumbaku na maziwa za Kenya zinaweza kuingia kwenye soko la Tanzania bila vizuizi, huku gesi na ngano ya Tanzania zikiweza kuingia Kenya bila vizuizi visivyohitajika.

Uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara kati ya Kenya na Tanzania uliathiriwa kwa muda huku mataifa yote mawili yakiweka marufuku hizo.

Marufuku ya bidhaa kutoka Tanzania kuingia Kenya ilitokana na wasiwasi wa kiusalama na ubora wa bidhaa huku Tanzania ikijibu kwa kuweka marufuku kwa bidhaa za Kenya kama vile matairi ya gari, mafuta ya kupaka mkate na maziwa.

Tanzania pia imepiga marufuku usafirishaji wa maindi kutoka Zambia kuelekea Kenya, ambayo inakabiliwa na wakati mgumu wa ukosefu wa zao hilo muhimu.

Marufuku hizo, ikilingamishwa na idadi kubwa ya bidhaa zinazotoka na kuingia katika nchi hizo zinaweza kuathiri pakubwa biashara.

Katibu wa viwanda na uwekezaji nchini Tanzania Adolf Mkenda awali alikuwa amesema kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa kutoka Nairobi tangu mwezi Februari na Juni wakati mataifa hayo mawili yalipokubaliana kwamba marufuku hizo ziondolewe.

0 comments:

Post a Comment