Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Monday, October 9, 2017

Balozi Dokta Mahiga kumpokea Mtukufu Aga Khan hapo kesho.



Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete enzi za utawala wake  akiongea na Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Mtukufu Aga Khan akiongea baada ya kumkabidhi hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan. Picha na maktaba.

Mtukufu Aga Khan, Imamu  wa Waislamu wa Shia Ismailia atawasili nchini Jumatano, Oktoba 11 na atapokewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga.

Kiongozi huyo wa kiroho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), atawasili nchini ikiwa ni kituo cha pili cha safari yake ya Afrika Mashariki.

Aga Khan leo Jumatatu amewasili Kampala nchini Uganda ambako amehudhuria siku ya uhuru kwa mwaliko wa Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.



Mratibu wa Mawasiliano wa Baraza la Aga Khan, Aly Ramji katika taarifa iliyotolewa leo amesema ziara hiyo ya siku mbili ni kwa mwaliko wa Rais John Magufuli.

Akiwa nchini amesema pamoja na mambo mengine atakutana na wanachama wa jumuiya yake.

Ramji amesema ni sehemu ya mzunguko wa ziara unaofanana na ukumbusho wa Jubilee ya Aga Khan ya Diamond - ambayo inaashiria miaka 60 kama kiongozi wa kiroho wa Jumuiya ya Waislamu wa Shia Ismailia.

Mbali na jubilee amesema wamekuwa na fursa ya kuzindua au kuendeleza miradi ya maendeleo ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi ikiwemo ya hospitali, shule, vyuo vikuu na taasisi za fedha ambazo hutumikia watu wa asili na imani zote.

Taarifa hiyo imesema Mtukufu Aga Khan ni mwanzilishi na mwenyekiti wa AKDN ambao ni mtandao wa kimataifa unaojitolea kuboresha maisha ya watu wote. @mcl

0 comments:

Post a Comment