Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Thursday, October 12, 2017

KATIBU MWENEZI WA CCM MANISPAA YA IRINGA: WAPINZANI MJIPANGE VILIVYO KUENDELEA KUWA MADARAKANI

 Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo sabasaba manispaa ya Iringa.



Na Fredy Mgunda,Iringa. 

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Edwin Bashir amewataka wapinzani kujipanga

vilivyo kwa kuwa amechaguliwa kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi na wananchi wa manispaa wanakuwa na imani na kukirudisha chama hicho madarakani katika 
chaguzi zote zitakazo jitokeza hapo baadae.
Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Bashir

alisema kuwa atahakikisha anakieneza chama vilivyo ili kuongeza wanachamawanaokipenda chama hicho.
“Mimi mwenezi hivi nilivyo nitakieneza chama kwa nguvu zote kwasababu tunavijana na viongozi wa kuleta mabadiliko ndani ya chama hata mkisema ninyoe nywele nitanyoa(hata wakisema

tumooge mafwiri tumoga eeela) kwa lengo la kuhakikisha tujakijenga chama kuwa chama 
cha wananchi” alisema Bashir
Bashir aliwataka wanachama kushikana kuahakikisha wanakuwa wamoja ili kuongeza wanacha wengine na kuendelea kuimalisha jumuhiya zote za chama hicho za  manispaa ya Iringa.
“Bila kuwa na umoja hatuwezi kwenda mbali wala kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mmenichagua kuwa

mwenezi hivyo nitaifanya kazi yangu kwa moyo wangu wote” alisema Bashir
Aidha Bashir aliwashukuru wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa na imani naye na kuhakikisha amekuwa mwenezi hivyo ametoa pongezi kwa wale waote waliomchagua kwa kura

nyingi.
“Mmenifanya niwe na furaha sana maana sio kwa wingi wa zile kura mlizonipa na kunifanya leo hii nasimama kama mwenezi kwa ajili ya kura zenu sasa subirini kazi yangu ya kukieneza chama na naomba tusahau yote yaliyopita na 
kuhakikisha tunaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Bashir
Naye katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marko Mbago alimpongeza Edwin Bashir kwa ushindi alioupata na kumuomba kukieneza chama kwa nguvu zote hata kwa kuutumia

umaarufu wake kuongeza wanachama ambao watakitumikia chama hiki hapa manispaa.
“Wewe ni maarufu na unapendwa sana hivyo tunatengemea mengi kutoka kwa kutokana na uzoefu wako wa kuishi vizuri na wananchi wa manispaa ya Iringa na kuijenga CCM mpya hapa manispaa” alisema Mbago
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa sasa ni

muda mwafaka wa kuongeza wanachama wapya na kuimarisha jumuhiya zote hapa manispaa ili kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi ya kushinda tena.
“Mimi nakufahamu muda mrefu sasa tumia vijana wako wote ambao umewapa mafanikio kwa muda mrefu kukurudisha

fadhila na kukuunga mkono katika harakati zako za kisiasa” alisema Rubeya
Ritta Kabati ni mbunge wa viti maalam mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alimpongeza mwenezi Edwin Bashir kwa ushindi alioupata lakini akawataka viongozi wengine

kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika haraka zake za kueneza chama.

 “Kufanya kazi pekee yake hawezi kupata matokeo chanya hivyo ni lazima sisi viongozi na wanachama kumpa ushirikiano wakutosha kuhakikisha mikakati yake inaenda vile chama kinataka na

kuahikisha anaijenga CCM mpya hapa manispaa ya Iringa” alisema Kabati

0 comments:

Post a Comment