Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Tuesday, October 10, 2017

LHRC YATAJA SABABU ZA KWANINI SERIKALI IIFUTE HUKUMU YA KUNYONGWA.

Kwa mara ya 15 leo Ulimwengu unaadhimisha siku ya kupinga adhabu ya kifo ambayo hutolewa na Mahakama kwa wanaokutwa na hatia huku mwito zaidi ukielekezwa kwa serikali za mataifa ambayo yangali yanatekeleza adhabu hiyo kuipa kisogo.
Maadhimisho ya mwaka huu yaliyobeba ujumbe mkuu usemao umasikini na haki ni mchanganyiko hatari yanajiri wakati ambapo mataifa ambayo hutua adhabu hiyo yameongezeka matharani katika mwaka 1976 nchi 16 tu zilifuta adhabu ya kifo,lakini hii leo nchi 133 ama zimeondosha kabisa au kisheria, zimepiga marufuku adhabu hiyo.Miongoni mwa nchi hizo 91 zimefuta kabisa adhabu ya kifo.Wakati huo huo katika nchi 64 bado adhabu ya kifo inaendelea kutumika.

fuatilia tamko la kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC katika siku hii.



video kwa hisani ya LHRC

0 comments:

Post a Comment