Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto
 Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii akiwa nyumbani kwake 
jijini Dar es salaam  na amepelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe. 
 
Taarifa
 fupi iliyotolewa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis, 
amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo huku akibainisha kwamba sababu
 za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake 
aliyoitoa juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini 
Dar es salaam katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa 
madiwani kwenye kata 43 nchini.
 
 
 
0 comments:
Post a Comment