Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Tuesday, November 7, 2017

HUYU NDIYE MGHANA ALIYETEMWA NA AZAM FC.



Klabu ya soka ya Azam FC imetangaza kuachana na nyota wake wa kimataifa Yahaya Mohamed kutoka nchini Ghana baada ya kushindwa kuonesha kiwango cha kuridhisha.

Taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa viongozi wamekaa na mchezaji huyo na kumalizana vyema kwasababu pande zote mbili zinatambua changamoto za mchezo wa soka kuwa kuna mazingira kugoma lakini pia falsafa kutoendana na mchezaji.

Aidha klabu hiyo imesema itaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa Yahaya alioutoa kwenye timu hiyo hususani kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambapo aliisadia klabu kuibuka mabingwa.

Yahaya ataondoka nchini kesho kurejea kwao Ghana. Azam FC imesema itaanza mapema mchakato wa kumpata mrithi wa Yahaya ambaye atasajiliwa wakati wa dirisha dogo kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu.

Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 19 nyuma ya Simba SC ambayo pia ina alama 19 zikitofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.

0 comments:

Post a Comment