Polisi Zanzibar imesema imepokea taarifa ya kuzama kwa boti katika Bahari ya Hindi iliyokuwa ikitokea Tanga kuelekea Kisiwa cha Pemba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji akizungumza na MCL Digital
leo Alhamisi Novemba 30,2017 amesema wamepokea taarifa leo asubuhi
kutoka kikosi cha KMKM ambacho ndicho chenye dhamana ya kufanya msako na
doria katika Bahari ya Hindi eneo la Zanzibar. Amesema wanaendelea na
ufuatiliaji .
“Wenzetu wa KMKM wameanza utafutaji wa
boti hiyo ambayo hatuijui jina wala ilikuwa na kitu gani na idadi ya
watu waliokuwamo,” amesema.
Kaimu Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga, Leon Rwegasira amesema boti hiyo ilikuwa na watu watano
akiwamo nahodha na ilikuwa imebeba mifuko 900 ya saruji ikitokea Tanga
kuelekea Zanzibar.
Ofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri
wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Tanga, Dk Walukani Kulyamba
amesema taarifa kamili zitatolewa zitakapothibishwa.
Awali,
Shirika la Habari la AFP lilisema watu tisa hawajulikani waliko baada
ya boti waliyokuwa wakisafiri kuzama katika Bahari ya Hindi.
Shirika
hilo limesema boti hiyo ilikuwa ikisafirisha vifaa vya ujenzi ikiwemo
saruji na ilikuwa na wafanyakazi watatu na abiria sita.
0 comments:
Post a Comment