Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

Labels

Wednesday, November 8, 2017

Mlipuko unaosadikiwa kuwa wa bomu umeua wanafunzi watatu wilayani Ngara.


Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu umeuwa wanafunzi watatu wilayani Ngara mkoani Kagera na kujeruhi wengine kadhaa katika shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara Mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba wanafunzi hao walikuwa wakati wa mapumziko ya saa nne, na ndipo mlipuko huo ulipotokea na kusababisha madhara makubwa ya vifo..

Jeshi la polisi tayari lipo eneo la tukio kufuatilia na kufanya uchunguzi, na taarifa kamili zitatolewa baada ya muda mfupi.

0 comments:

Post a Comment