Dar es Salaam. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama
cha Walimu Tanzania (CWT), Yahya Msulwa amefariki dunia jana katika
Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Gratian Mkoba ameithibitisha Mwananchi leo Ijumaa Novemba 17 wakati akizungumza kwa simu.
Mkoba
amesema, “Ni kweli amefariki jana usiku na alipelekwa jana hiyo usiku
kwa mujibu wa ndugu zake walionipa taarifa, maana mimi nilikuwa nina
wiki moja hatujawasiliana na sijui alikuwa na anasumbuliwa na
nini,”amesema Mkoba.
Amesema hivi sasa yupo njiani kwenda nyumbani kwa marehemu Tuangoma kujua taratibu za mazishi.
0 comments:
Post a Comment