Harare, Zimbabwe. Viongozi wa chama tawala cha
Zanu PF wanakutana leo kuandaa rasimu ya uamuzi wa kumwondoa madarakani
Rais Robert Mugabe mwishoni mwa wiki hii.
Pia,
wataandaa mazingira ya kumfungulia mashtaka wiki ijayo ikiwa ataendelea
kukataa kuachia madaraka, kiongozi wa ngazi ya juu amesema.
"Hakuna
kurudi nyuma," kiongozi huyo aliliambia shirika la habari la Reuters.
"Ikiwa atazidi kuwa mkaidi, tutaandaa mazingira ili afukuzwe Jumapili.
Hilo likifanyika atafunguliwa mashtaka Jumanne."
Hatima
ya Mugabe bado haijulikani hadi leo kwani imeelezwa amekataa juhudi
zote za kumtaka ajiuzulu baada ya jeshi kutwaa mamlaka ya nchi ambalo
hadi wiki hii lilikuwa nguzo muhimu katika utawala wake wa miaka 37.
Jeshi
lilisema kupitia televisheni ya taifa kwamba lilikuwa linafanya
mazungumzo ili kupata ufumbuzi na kwamba litaliarifu taifa kuhusu
matokeo haraka iwezekanavyo.
Marekani, mkosoaji wa
miaka mingi wa Mugabe kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na wizi wa
uchaguzi inataka “enzi mpya” Zimbabwe, alisema ofisa wa ngazi za juu wa
mambo ya nje wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika ukiwa ni wito uliowazi
wa kumtaka mzee huyo aondoke.
Mkanganyiko umejitokeza
pale Mugabe alipoonekana jijini Harare kwenye picha akiwa mtu mwenye
tabasamu na akisalimiana na mkuu wa majeshi wa Zimbabwe, mtu ambaye yuko
nyuma ya mapinduzi na kuibua maswali kuhusu kukaribia mwisho wa enzi
zake.
Katika hali isiyotarajiwa Mugabe aliondoka kwa
msafara kwenye nyumba yake ya kifahari maarufu kama "Paa la Bluu"
alikokuwa amezuiliwa na jeshi na akaenda hadi Ikulu ambako alipigwa
picha zilizosambabzwa kwenye vyombo vya habari alikutana na mkuu wa
majeshi, Jenerali Constantino Chiwenga na wapatanishi kutoka SADC.
0 comments:
Post a Comment