Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa African news tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Jim Media Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Labels

Thursday, February 22, 2018

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MAHAFALI YA 34 YA CHUO KIKUU HURIA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewakumbusha wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuwa Vyeti walivyotunukiwa ni tuzo halali kwa juhudi na jitihada walizoonesha darasani.
Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa sherehe za mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri Bariadi mkoani Simiyu.

Makamu wa Rais alisema “ Jamii inategemea mtaipatia tuzo ya utendaji bora na ufanisi katika fani zenu utakao akisi viwango vilivyoainishwa kwenye vyeti vyenu”.

Makamu wa Rais aliupongeza uongozi wa chuo kwa jitihada zake katika kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais hasa katika sula la Uchumi wa Viwanda ambapo chuo hicho kimefanya Kongamano kubwa la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda mjini Bariadi lakini pia chuo hicho kipo kwenye mchakato wa Kigoda cha kiprofesa cha Viwanda na Maendeleo.

Makamu wa Rais aliwakumbusha uongozi wa chuo katika jitihada zake za kutekeleza majukumu ya chuo , uendelee kujikita kwenye kauli mbiu yake Elimu Bora na Nafuu kwa Wote .

Katika Mahafali hayo ambayo zaidi ya wanafunzi 941 wamehitimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na nchi za jirani ambapo wanafunzi saba (7) walihitimu Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu Huria.

Tuesday, February 20, 2018

TANZANIA YAZIDI KUNAWILI KIUTALII KENYA YAKIRI.

Kenya imekiri kuwa imekuwa ikipoteza watalii kwenda Tanzania miaka ya hivi karibuni.

Akizungumza kwenye kituo cha runinga ya Citizen nchini Kenya, waziri wa utalii nchini Kenya, Najib Balala, aliezea wasi wasi kuhusu hali ya mahoteli nchini Kenya, akisema kuwa ukosefu wa hoteli za viwango vya kimataifa nchini Kenya imechangia Tanzania kuwa chaguo la watalii kanda hii ya Afrika Mashariki.

"Sababu ambayo ilichangia Tanzania kufanya vyema kutuliko mwaka 2017 ni kwa sababu hoteli zao ni mpya na za kisasa wakati hoteli zetu zikiwa ni za miaka 40 iliyopita," alisema Balala.


Balala alisema kuwa licha ya idadi ya watalii wanaowasili Kenya kuongezeka kutoka 1,342,899 mwaka 2016 hadi 1,474,671 mwaka 2017, Kenya ina uwezo wa kuwavutia watalii zaidi ikiwa hoteli na huduma kwa wateja zitaboreshwa.

"Changamoto kubwa tuliyo nayo sasa ni usalama. Mpaka wetu na Somalia pia unaleta wasiwasi na hofu kwa wageni wetu," alisema Balala.

Balala alisema kuwa Kenya inalenga kuwavutia watalii milioni 2.5 kila mwaka ifikapo mwaka 2022, akiongeza kuwa serikali imefanya mazungumzo na wamiliki wa hoteli kuhusu viwango ambavyo hoteli zinastahili kuwa navyo.

Idadi ya watalii wa kigeni wanaozuru Tanzania imekuwa ikipanda tangu ivuke watalii milioni moja kwa mwaka kwa mara ya kwanza mwaka 2012.

Kulingana na wizara ya utalii, watalii 1,137,182 waliingia nchini Tanzania mwaka 2015 na idadi hiyo ikapanda hadi watalii 1,284,279 mwaka 2016.

Utalii uliiletea Tanzania dola bilioni 2.3 mwaka uliopita kutoka dola bilioni 2 mwaka 2016. Mapato ya mwaka 2015 yalikuwa ni dola bilioni 1.9.

Monday, February 19, 2018

FAO launches guide to tackle Fall Armyworm in Africa head-on Fighting FAW in an integrated, ecological and sustainable way


Rome - Faced with the infestation of millions of hectares of maize, most in the hands of smallholder farmers, and the relentless spread of Fall Armyworm (FAW) across most of Africa, the UN Food and Agriculture Organization (FAO) launched today a comprehensive guide on the integrated pest management of the FAW on maize.

The guide was developed with a host of partners: International Institute of Tropical Agriculture (IITA), International Centre of Insect Physiology and Ecology (ICIPE), Lancaster University, Centre for Agriculture and Bioscience International (CABI), Empresa Brasileira de Pesquisa Agropecuária (EMBRAPA), Colegio de la Frontera Sur (ECOSUR) and the United States Department of Agriculture (USDA).Photo: ©FAO/Rachel Nandalenga

It will help smallholder farmers and frontline agricultural staff to manage FAW more effectively amidst fears that FAW may push more people into hunger. Central and Southern Africa are particularly on high alert, as the main maize growing season is currently underway in these regions.

Based on a learning-by-doing approach and designed for Farmers Field Schools, the guide is packed with hands-on advice. It provides support for a correct identification of this new foe for African farmers, and offers options to manage it in an integrated, ecological and sustainable way.

"We know that farmer education and community action are critical in best managing FAW, and curbing its spread as much as possible," said Maria Helena Semedo, FAO Deputy Director-General.

"The guide builds on the experiences of farmers and researchers from the Americas who have been dealing with the pest for centuries as well on new technology and lessons learnt so far in Africa. It gives African farmers and frontline agricultural workers the practical advice they need to tackle FAW head-on," added Semedo.

FAO also calls on those African countries likely to be affected soon, given the current distribution of FAW in Africa, to get prepared by: re-enforcing early warning systems at community level, raising awareness among farmers, and using available materials, such as the guide.

By early 2018, only 10 (mostly in the north of the continent) out of the 54 African states and territories have not reported infestations by the invasive pest.

The Guide on Integrated Management of the FAW on maize up close

"As FAW is new to Africa, farmers' and crop protection and extension workers' good understanding of the pest's behavior and management practices are crucial in effectively managing it without damaging human health and the environment," said Bukar Tijani, FAO Assistant Director-General and Regional Representative for Africa.

Key guidelines and advice on effectively and sustainably managing FAW include:

Visit the field and look at the status of the crop: its health and signs of presence of the FAW. Farmers can take direct action by crushing egg masses and young larvae.
FAW damage can look alarming, but maize plants have a good capacity to compensate for that damage and often little yield is lost.
Learn about FAW behaviour. For example: understanding how and where the adult female moth lays her eggs can help determine where to plant mixed crops to prevent further spread of FAW.
Understand the important role of natural biological control in managing FAW. Studies have shown that FAW suffers up to 56 percent mortality from parasitoids (beneficial insects such as tiny wasps killing eggs or larvae of the FAW) alone.
Farmers must be able to recognize the FAW natural enemies and learn how to conserve and enhance them. Ants have already shown to be important FAW predators.
Fields in Nigeria have already shown high levels of natural FAW mortality due to fungal and viral entomopathogens (pathogenic organisms killing FAW larvae). Farmers can ‘recycle' these naturally-occurring pathogens.
Farmers can try "local remedies", including application of ash, lime, sand, or soil directly into infested whorls, already successfully used by some African farmers against FAW.
Pesticides versus bio-pesticides: what should be used to fight FAW?

The guide recommends that at a national policy level, information and recommendations regarding the role of pesticides in FAW management are urgently needed.

The guide warns that insecticide applications are costly, may not work because of resistance, poor application techniques, or low-quality pesticides, and will negatively affect FAW's natural enemies.

Although farmers may receive insecticides free this year, and maybe next, it is doubtful if they will still be receiving them in the longer-term. Alternative and sustainable solutions must be found as FAW is in Africa to stay and will be infesting maize fields for many years.

The actions taken to date in most countries have been limited to the use of synthetic pesticides (especially organophosphates, synthetic pyrethroids, a few neonicotinoids, and in some cases cocktails of pesticides). In some countries, the pesticide applications were mainly emergency responses, not based on a cost-benefit evaluation.

Older pesticide molecules, recognized as hazardous and banned in industrialized countries, are often still readily available and widely used in African countries. These products put farmers' health and their environments at risk. Their use may also result in pesticide residue levels that could jeopardize the marketability of crops both on domestic and export markets.

Bio-pesticides, including those based on bacteria, virus, and fungus have been tested, developed, registered and used successfully in the Americas.

The use of botanical and biological insecticides (certain strains of Bacillus thuringiensis (Bt), fungi and virus) to manage FAW has been reported to be effective in several sources, but bio-pesticides are not always locally available in the affected countries.

Tackling FAW

Farmer Field Schools have been supported by FAO for over twenty-five years and have proven an effective approach to reaching millions of smallholder farmers and successfully engage them in a learning process resulting in better management of their crops and natural resources.

FAO has been already rolling out Training of Trainers on how to manage FAW for frontline crop protection and extension in countries most affected by FAW.

"With this guide, FAO will begin a continent-wide program of training master trainers to initiate an All-Africa Programme of Farmer Field Schools for the sustainable management of FAW. Over the next five years, FAO and partners aim to reach 10 million farmers through 40,000 Farmer Field Schools across Africa," said Allan Hruska, FAO Principal Technical Coordinator on Fall Armyworm.   

Work is also underway to launch a FAW Monitoring and Early Warning System (FAMEWS) app in Madagascar, Zambia, and South Africa, and then gradually roll-it out across the continent. Already tested, the FAO app will enable farmers to send vital info about their crops' health, helping to generate detailed and reliable knowledge on FAW infestation levels, FAW adult population levels, and on the outcomes of actions taken against FAW.

FAO and its partners have been at the forefront in tackling FAW, and continue to support prevention, early warning and effective response.

In addition to the FFS guide and its roll-out across Africa, FAO took immediate steps as soon as FAW was detected in Africa by: bringing together experts to share knowledge and experiences on sustainable FAW management; giving farmers and frontline agricultural workers the understanding, experience and confidence to tackle FAW; supporting countries to mitigate pest damage, develop action plans, and train extension workers and farmers.

FAO also developed a Framework for Partnership for sustainable management of FAW to provide guidance for the development of FAW-related projects and programmes and ensure synergies and complementarities among the different development partners.

Tanzania sets record in potato research, to release improved varieties.


By Zephania Ubwani @ubwanizg3

Tanzania has excelled in experimental trials of high yielding and disease resistant potato varieties under a climate smart agriculture programme aimed to improve food security.

Three of 14 varieties brought into the country by the International Potato Centre (CIP) for field trials in Lushoto district did well and two of them will soon be released toThese are Unica, locally known as Mkanano, and Shangii which will be released to farmers for cultivation after proving resilience to climate vagaries.

The third variety, Mvono, is now with the Tanzania Official Seed Certification Institute (Tosci) for national performance trials in the southern highlands regions.

"Mvono is being tested for the first time in the world. Its first field trials are taking place in Tanzania", said Dr Stephano Sebastian, the principal agricultural research officer with HORTI-Tengeru.

Experimental trials and promotion of potato is one of the projects implemented within the East African region under the Consultative Group on International Agricultural Research (CGIAR) research programme on climate change, agriculture and food security (CCAFS).

Within the region, the global programme, launched in 2010, encompasses Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda and Ethiopia.

In Tanzania, the focus is to develop more resilient potato varieties with higher yields.

Dr Sebastian said the project involving 600 families in five villages in Lushoto district, will ultimately phase out 'Kidinya', a low yielding local potato variety which is susceptible to blight disease.

"To address these issues, the CGIAR research programme on climate change, agriculture and food security initiated a study aimed at developing more resilient potato varieties that can give higher yields", he said.

Besides the Peru-based CIP, other partners in the project include the Selian Agricultural Research Institute (Sari), Lushoto district council, YARA Tanzania Limited, NGOs and the Lushoto farmers.

Based on demand by Lushoto farmers, the project also sought to develop potato varieties with better culinary traits, the expert explained in an interview.

The trials were carried out at Kwesine, Boheloi, Maringo, Kwekitui and Milungui villages with experimental materials comprising of six advanced and heat tolerant clones from CIP.

"The origin of the project stemmed from addressing the vagaries of weather. One of the challenges facing the farmers is unpredictability of rains, viral diseases and knowledge deficiency", says CCAFS project leader, Dawit Solomon.

Under the programme, in Rwanda farmers are turning to locally-tailored climate forecasts to help them make farming and investment decisions, he said.

Monday, February 5, 2018

Dk.Mwigulu aiagiza Polisi Pangani kudhibiti wahamiaji Haramu.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwamba taasisi hiyo ndiyo inayoshughulika na haki za watu na wasipofanya kwa uadilifu yapo madhara makubwa kwa jamii na kutoka kwa wahalifu. 
Akizungumza  katika uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha polisi Wilaya ya Pangani, Dk Mwigulu amesema kuwa wilaya ya Pangani ni lango ambalo wahalifu hasa wahamiaji haramu hupitia kwenda kusini mwa Tanzania. 

‘’Kamateni wahalifu wote wanaoingia kimagendo au wanaoingiza mizigo kimagendo hakuna mjadala kamateni na wafikisheni katika vyombo vya sheria ,’’amesema Dk Mwigulu.

Kwa mujibu wa Dk Mwigulu, Mikoa ya kaskazini mwa Tanzania inaongoza kwa kuingiza wahamiaji haramu na bidhaa kwa magendo kwasababu ipo mipakani hivyo kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi hizo.

‘’Ujenzi huu wa kituo cha polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama zaidi hivyo mimi nitachangia nondo 150 baada ya mifuko 450 ya cement kupatikana basi ujenzi uanze haraka iwezekanavyo na kituo kiwe cha hali ya juu kikubwa.’’ amesisitiza

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wilaya hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa polisi Christina Musyani amesema kuwa wilaya hiyo ina vituo vitatu pekee vya polisi ambavyo havitoshi na mazingira yake hayaridhishi.

Amesema wameamua kuanza ujenzi wa kituo hicho ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa sasa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta vituo vya polisi.

"Kwa kushirikiana na wananchi, Mbunge na halmashauri tumeamua kuanza ujenzi wa kituo cha kisasa ,’’ amesema Christina.

Tuesday, January 23, 2018

Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza

Watu  wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine wanane kujeruhiwa vibaya katika ajali ya mabasi mawili yakugongana uso kwa uso katika kijiji cha Kamanga, Sengerema mkoani Mwanza saa nne asubuhi jana.

Akizungumzia ajali hiyo, shuhuda aliyekuwa katika pikipiki na kunusurika kugongwa na mabasi hayo, Philipo Budeba, alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi yote mawili.

“Mimi nilikuwa naendesha pikipiki, mbele yangu kulikuwa na basi la Mkombozi Trans lenye namba T540 DLF na nyuma kulikuwa na Basi la Walawi Express lenye namba T167 CSN yote yalikuwa na mwendokasi," alisema Budeba.

"Dereva wa Mkombozi ndiye aliyetaka kupita gari lingine, lakini ilishindikana na kusababisha magari hayo kuvaana... mimi nilijirusha kwenye kilima cha pembeni mwa barabara."

Naye abiria wa Mkombozi Trans iliyokuwa ikitokea Kanyara Buchosa, Sengerema, Fransisco Kansola alisema tabia ya madereva kushindwa kuchukua tahadhari na kujali kuwahi abiria ndiyo chanzo cha ajali hiyo.

Walawi Express lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Nemba wilayani Biharamulo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema dereva wa basi la Walawi, Frank Kimboka ni miongoni mwa majeruhi wanane wa ajali hiyo baada ya kujeruhiwa miguu yote.

“Waliofariki ni dereva wa basi la Mkombozi Trans aliyefahamika kwa jina la Simon Mdalesalamu na mwanamke aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20," alisema Kamanda Msangi.

Majeruhi watatu wametajwa kuwa ni Frank Mushi aliyevunjika miguu yote miwili, Isaack Hamisi (22) mkazi wa Nyasaka wilayani Ilemela na Mwinyi Ismail (50) aliyevunjika miguu yote miwili, alisema Kamanda Msangi.

"Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi hayo.”

Aidha, ajali hiyo ilitokea wakati mkoa wa Mwanza ukizindua maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, yenye kaulimbiu inayosema ‘Zuia ajali, tii sheria, okoa maisha'.

Majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Rufani ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu.

MBUNGE MGIMWA NIPO TAYARI KUNYIMWA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2020.


Mbunge wa
jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa  akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.

Na Fredy Mgunda, Iringa Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.

Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.

Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao  kwa ajili ya faida ya maisha yao.

“Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo
ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwaalisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa.

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa
kuwa sheria itachukua mkondo wake.“

Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwaaliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.

“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

nao baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema walimu

Walimu walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.

“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Walimu.

Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu.

Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi

RAIS wa Zanzibar Dk. Shein Azungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)

DSC_5593
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
DSC_5612
VIONGOZI wa Ngazi za juu wa Serikali ya Abu Dhabi wakihudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa makaazi wa Mfalme wakati wa mkutano huo.(
DSC_5624
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)wakiwa katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi. kulia Balozi wa Tanzania Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Mbarouk Nossor Mbarouk.
DSC_5642
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mwenyeji wake , Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE), baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa makadhi ya Kiongozi huyo Nchini Abu Dhabi.
DSC_5656
Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE)akimtambulisha Mtoto Aaliyah Al Mansoori kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohahed Shein, wakati wakitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza mazungumzo yao
DSC_5681
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) wakitoka katika Jumba la Kiongozi huyo baada ya kumaliza mazungumzo yao
DSC_5711
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika makaazi ya Kiongozi hiyo Nchini Abu Dhabi.
Picha na Ikulu