Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani



Kwa habari za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiburudani

HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

HABARI ZA MICHEZO

Sasa African news tunakuhakikishia kupata taarifa zote za kimichezo kutoka viwanja mbalimbali duniani, lengo ni kuhakikisha hupitwi na lolote katika ulimwengu wa michezo.Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

TAARIFA ZA BURUDANI NA HABARI ZA WASANII

Unapenda masuala ya burudani? Ni jukumu letu kuhakikisha unazipata info zote za burudani na wasanii wanaokupa burudani, unapata video mpya, movie pamoja na muziki. Kaa karibu nasi.

KURASA ZA MAGAZETI KILA SIKU

Tunakupatia kila ambacho kinaandikwa katika magazeti ya Tanzania na nje ya Tanzania, usitie shaka ukishindwa kununua gazeti uipendalo, sogea karibu nasi na upate kila unachokihitaji.

MAHUSIANO

Fahamu mambo mengi katika ulimwengu wa mapenzi kwa kupitia dondoo, simulizi na visa mbalimbali kupitia Jim Media Online, Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Labels

Saturday, April 14, 2018

Harmonize Ft. Diamond Platnumz - Kwangwaru





MFAHAMU VEMA RAIS MPYA WA TLS, FATMA KARUME.

Mwanasheria mkongwe, Fatma Karume, ameshinda nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Fatma, ambaye licha ya kuwa mwanachama wa TLS kwa muda mrefu, lakini pia ni mtoto wa Rais wa sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Zoezi la kupiga na kuhesabu kura lilianza tangu asubuhi leo Aprili 14, mjini Arusha na likakamilika jioni huku Fatma akiibuka na kura  820 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Wakili Godwin Ngwilimi, aliyepata kura 363.

Wagombea wengine wa nafasi ya urais wa TLS walikuwa ni Godwin Mwapongo aliyepata kura 12 na Godfrey Wasonga, aliyepata kura sita.

Fatma ni nani?

Fatma Karume amezaliwa Juni 15, 1969, visiwani Zanzibar,

Ni Mtoto wa rais wa sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

Ni mjukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume.

Ni mwanasheria katika kampuni ya uwakili ya IMMA Advocates

Ni mwanzilishi wa kampuni ya uwakili ya Karume and Co Advocates 2004.

Fatma amewahi kuwa mwanasheria wa mwanasiasa Tundu Lissu katika kesi yake ya uchochezi, Julai mwaka jana.

Ofisi za kampuni ya uwakili ya IMMMA zilizopo Upanga, jijini hapa, ziliungua moto Agosti mwaka jana.


⧭Elimu Yake.

Degree of the Utter Bar, Middle Temple, London, 1998 Postgraduate Diploma in Professional Legal Skills, Inns of Court School of Law, 1998 LLM, London School of Economics, 1997 Diplome de Sciences Juridiques, Universite de Strasbourg, 1991 LLB (Hons), University of Sussex, 1992

AZAM WAIOMBA TFF WASOGEZA MBELE MECHI YAO DHIDI YA NJOMBE MJI




Na Agness Fracis,Blogu ya Jamii

UONGOZI wa Azam FC umeomba mchezo wao dhidi ya Njombe Mji usogezwa mbele kutokana na muda mchache waliopumzika baada ya kumalizana na Ruvu Shoting ya Mlandizi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Azam Jaffary Maganga amesema wameomba mchezo kusogezwa mbele
ili kupata nafasi ya kujiandaa ikiwa ni jana wametoka ugenini kucheza na timu ya Ruvu shooting.

"Tumeandika barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania( TFF) kuomba mchezo dhidi ya Njombe Mji ya mkoani Njombe usogezwe mbele badala ya kuchezwa kesho ikiwa sheria za FIFA zinasema inatakiwa kupumzika saa 72 na si 48,"amesema.

Mchezo huo uliotarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Azam Complex Chamazi.Ambapo kikosi hicho kimeendelea kujifua na mazaoezi kukabilia na Njombe Mji katika mchezo wao ujao.

"Tumerejea jana usiku kutoka Uwanja wa Mabatini Mlandizi tulipomaliza tu mechi na kikosi kipo mazoezini kujiandaa nadhani najua Njombe Mji ni timu nzuri pia"amesema Jaffary Maganga.

Azam FC walikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ruvu Shoting na kuendelea kubaki nasafi ya 3 wakiwa na alama 45,huku vinara Simba wakiendelea kujikita Kileleni kwa alama 52 na Mabingwa watetezi Yanga wao wakishikilia nafasi ya pili kwa pointi 47,katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Monday, March 19, 2018

Jinsi ya kufanya ili mtoto apende chakula.


Wazazi wengi hasa waishio mijini wanakumbana na changamoto ya watoto wao kutopenda kula ama kwa kukosa hamu na hata vinginevyo. Tumepata wasaa wa kuzungumza na mtaalamu wa lishe kutoka Shirika la Chakula Dunia (WFP), Neema Shosho na hapa tutakupa machache juu ya nini ufanye mwanao apende kula.

Shosho anashauri kwamba wakati wa kumlisha mtoto ni vyema mzazi au mlezi utumie lugha ya upole na upendo ili kumuhamasisha mtoto kula. Lugha za matusi, vitisho na ukali humfanya mtoto achukie na akatae kula chakula.

Kwamba ili mtoto apende kula, pendelea kumpa chakula chake kipindi ambacho familia pia inakula. Hii itamuhamasisha kula zaidi. Asile peke yake mara zote. Hata hivyo kumlisha mtoto kunahitaji uvumilivu. Tenga muda wa kutosha wa kumlisha mtoto wako. Ongea nae, zunguka nae na cheza nae huku ukimbembeleza kula kwa upole na upendo

Kamwe usijaribu kumkaba mtoto ili ale chakula. Hii inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo chakula kupita njia ya hewa jambo linaloweza kugharimu uhai wake. Vilevile kumkaba koo kunaleta madhara ya kisaikolojia wakati mtoto ataona kula ni adhabu na kuchukia chakula.

Jaribu kumpa mtoto vyakula vya aina mbalimbali ili ujue anapenda vyakula gani. Kwa watoto wakubwa kidogo mfano miaka mitatu na kuendelea ni muhimu kumshirikisha mtoto katika uandaaji wa chakula. Muulize angependa kula nini? Zungumza naye kama inawezekana kuandaa anachotaka mwambie na kama haiwezekani ajue kwa nini. Usimkaripie. Unampotezea uwezo wa kujiamini na ujenzi wa hoja. Nenda na watoto wako eneo unalonunulia chakula (gengeni, sokoni, supermarket, dukani, gulioni) na uwasikilize nini wanapendelea kula. Kumbuka mnaweza kufanya machaguo sahihi ya vyakula kwa bei nafuu kabisa.

Wewe mzazi au mlezi uwe kioo kwa mtoto wako kwa kula mlo kamili na wa bora. Mzazi ukila mlo kamili na wa bora ni rahisi mtoto kuiga na kupenda mlo wake. Vilevile jitahidi vyombo unavyotumia kumlishia mtoto viwe vinavutia. Usiweke chakula kwenye bakuli lililoharibika mfano lililoungua, lenye ufa, lililopondeka na kadhalika. Nunua vyombo vya watoto vizuri, vyenye kuvutia na vya bei nafuu kabisa ili kumuhamasisha mtoto kula.

Watoto wakubwa waruhusiwe kuingia jikoni chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi. Waonyeshe unavyoandaa chakula na washirikishe msaidiane kuandaa mlo kamili na ulio bora. Kumbuka kula mlo bora na kamili sio lazima uwe na pesa nyingi. Pangilia pesa uliyonayo na hakikisha unanunua vyakula bora, kamili na asili vinayopatikana kwenye eneo lako unaloishi

Alama 11 za mpenzi mwenye mchepuko.




Kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba uhusiano baina ya wapendanao ulikusudiwa kuwa ya upendo, maelewano, kuaminiana na urafiki wa hali ya juu. Kwa bahati mbaya hali halisi siyo hiyo katika mahusiano ya wengi. Wengi wetu wameumizwa kwa mpenzi mmoja au mara nyingine wote kutokuwa waaminifu katika mahusiano yao.

Kutokuwa mwaminifu hapa namaanisha hali ya mpenzi mmoja kuwa na mahusiano yasiyo rasmi na mpenzi au wapenzi wengine pembeni au mchepuko kwa lugha ya kisasa

Japo jambo hili hufanyika kwa siri sana kwa kuogopa kuharibu mahusiano mtu aliyonayo, wako baadhi ambao wamegundulika na mahusiano yakaathirika kwa kiasi kikubwa na wengine yalikufa kabisa.

Wako ambao wameweza kuhimili machungu ya kugundua hali ya wapenzi wao kutokuwa waaminifu lakini pia wako ambao imewashinda kabisa kuwa wavumilivu, wako ambao hali hii imewaletea shida kihisia, kisaikolojia na hata kiafya.

Kwa bahati mbaya wengi wetu hatuzijui hata dalili au alama zozote za kutujulisha mabadiliko waliyonayo wapenzi wetu ili basi walao tuanze mapema kufanya uchunguzi au kupeana tahadhari kabla makubwa na machungu zaidi hayajatokea.

Zifuatazo nia alama zitakazokusaidia kuwa macho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea katika uhusiano yenu, alama hizi nimezikusanya katika mazungumzo na baadhi ya watu niliowahi kusaidiana nao kutatua matatizo ya mahusiano yao na pia nikazihakikisha kupitia kusoma vitabu mbalimbali, kwa hiyo nina uhakika zitakusaidia kuona uhalisi wa mambo, na yamkini utaona baadhi ya alama ambazo umeshawahi kuzihisi au kuzishuhudia katika mahusiano yako.

Kuongezeka ghafla kwa hali ya kujipenda

Yawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa kawaida, hapa simaanishi kutopendeza, na wewe ulikuwa umemzoea katika hali fulani ya mavazi au mitindo mara ghafla anabadilika nakuwa mtanashati zaidi, ana badilisha mavazi, anapenda mavazi ya gharama, labda alikuwa hatumii manukato lakini ghafla anaanza kupenda manukato tena ya gharama, anakuwa mtu wa kujijali zaidi ya kawaida yake kiasi ambacho hukumzoea. Katika hali hii jaribu kuwa macho zaidi kufahamu nini kilicho sababisha mabadiliko ya ghafla kiasi hicho.

Kuanza kuchelewa kutoka kazini mara kwa mara

Sio kwamba kila mtu anapochelewa kutoka kazini basi anakuwa sio mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 ya ambao wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa hili.

Unaweza kukuta mtu alikuwa anafanya kazi hiyo muda mrefu tu tangia muanze mapenzi yenu, mara ghafla hali inabadilika, sikuhizi anachelewa sana kurudi nyumbani, na anaporudi unaweza kutegemea utamwona amechoka kimwili na hata kiakili kwa majukumu ya kazi kuhusiana na asili ya kazi anayoifanya lakini unakuta mtu wala haonyeshi kuchoka, ana furaha kama kawaida.

Hali hii inapojitokeza mara kwa mara usichelewe kufungua macho na kudadisi mazingira maana yamkini ni kweli amepata kazi ya ziada ila siyo ile ya ajira unayoijua wewe.

Kupenda kutembea na mipira ya kinga “condoms”

Inashangaza mara nyingine kusikia mpenzi mmoja ana tabia ya kubeba kondomu kwenye pochi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali, cha kushangaza zaidi unakuta yuko katika mahusiano na mkewe au mumewe. Yamkini ni kweli kunakujali na labda katika mahusiano yenu hili sio la kushtua kwa sababu mnajali afya zenu au mnatumia kondomu kwa sababu zaidi ya moja, lakini inakuwaje pale unapogundua kuwa ile kondomu uliyokuwa unaiona haipo tena na yamkini wewe hukuhusika katika kuitumia.

Mazingira tatanishi ya simu

Inawezekana mpenzi wako sio mtu wa kupokea simu au kupiga simu sana, na hivi ndiyo ulivyomzoea, mara ghafla simu zinaanza kumiminika mpaka mida ya usiku. Yamkini pia alikuwa yuko huru hata simu yake inapolia waweza ichukua na kumpatia lakini ghafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, nimeongea na wengine ambao wanakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika.

Wengine wameanza kuondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kuzipokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa lakini mtu uliyempenda na ukamzoea unaweza kugundua uhalisi wa anachokiongea kwenye simu na jinsia ya anayeongea naye kwa kumuangalia usoni tu.

Yamkini mpenzi wako amepigiwa simu na kwa sababu hakuwepo karibu ukaipokea, na mara mpigaji wa simu anapogundua aliyepokea sio mwenye simu anakata simu hiyo ghafla, au ghafla unagundua kila simu inayopigwa kwenye simu ya mpenzi wako haionyeshi namba au haionyeshi jina. Mazingira kama haya yanapozidi basi jaribu kuchukua hatua, yawezekana kuna mvamizi tayari katika mahusiano yenu.


Itaendelea

Mambo muhimu ya kuhakikisha usalama wako mvua inaponyesha.

Lori lililosombwa na amfuriko  Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Usalama Barabarani (NTSA) pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya wametoa ushauri ambao unaweza kukufaa sana wakati huu wa mvua.

  1. Fahamu kwamba wakati wa kiangazi, vumbi, mchanga na taka za aina mbalimbali hurundikana barabarani. Mvua inaponyesha, husababisha barabara kuwa telezi na kwa hivyo ukiwa na gari ni muhimu kutoendesha gari lako kwa mwendo wa kasi kupindukia kwani gari likiteleza utashindwa kulidhibiti gari lako kwa urahisi.
  2. Kwa sababu ya maji, huwa vigumu sana kupiga breki wakati wa mvua na hivyo hatari ya mwenye gari kumgonga anayetembea barabarani huwa juu. Unashauriwa kutoendesha gari kwa mwendo wa kasi.
  3. Kwa sababu ya mvua, wapita njia mara nyingi hutembea wakiwa wameinamisha vichwa chini na huenda wasilione gari linapokaribia. Wenye magari wanashauriwa kuwa makini zaidi wanapofika kwenye vivuko barabarani au wanapomuona mtu akivuka barabara. Kwa wanaotembea kwa miguu, wanashauriwa kutumia vivuko vilivyotengwa na kuchukua tahadhari zaidi pia.
  4. Kwa wenye magari, iwapo barabara imefurika maji, ni vyema kutafuta barabara nyingine ya kupitia badala ya kujaribu kupitia ndani ya maji. Huwa vigumu kukadiria kina cha maji barabara inapofurika.
  5. Wakati mvua inaponyesha, wenye magari wanatakiwa kuwasha taa kuwawezesha kuona mbele na pia kutokaribia sana magari yaliyo mbele yao. Maji yanayorushwa na gari lililo mbele yanaweza kutatiza mwenye gari iwapo atakuwa karibu sana. Ushauriwa kufuata kanuni ya sekunde 3, hicho ndicho kipindi kinachochukuliwa na binadamu kuona jambo na kuchukua hatua. Usipofanya hivi, kufikia wakati unapoona aliye mbele yako amesimama na kuchukua hatua utakuwa tayari umesababisha ajali.
  6. Breki za gari huathiriwa na maji, kwa hivyo unapoendesha gari eneo lenye maji, ni vyema kuendesha gari kwa mwendo wa polepole. Hii itaziwezesha breki kukauka.
  7. Madereva wanashauriwa pia kutumia mikono yao miwili kudhibiti mwelekeo wa gari kuhakikisha wanadhibiti vyema gari.
  8. Wapita njia, waendesha baiskeli na waendeshaji pikipiki wanashauriwa kuvalia mavazi yanayoweza kuonekana vyema au mavazi yanayoweza kuakisi mwanga. Haya yatamuwezesha mtu kuonekana na madereva na kumpungushia mtu hatari ya kugongwa.
  9. Usiendeshe gari lako ndani ya maji yanayosonga, yawe kwenye mifereji au kwenye mto. Huwa vigumu sana kukadiria nguvu ya maji. Magari mengi husombwa na maji madereva wakijaribu kuvuka mito au wakitumia madaraja yaliyofurika maji. Mvua pia hudhoofisha madaraja, jambo ambalo huenda usifahamu. Daraja linaweza kubomolewa bila ufahamu wake wewe nawe ukaingia mtoni ukitarajia daraja bado lipo. Maji ya kina ya futi moja yanaweza kusomba gari lako. Kwa binadamu anayetembea, inchi sita za maji zinaweza kukusomba.
  10. Ukiwa na gari lako, hakikisha vipangusia kioo vya gari lako vinafanya kazi. Hili litakuwezesha kupangusa kioo na kuona mbele unapokuwa barabarani.
  11. Iwapo una gari na limeanza kuteleza, achilia mafuta na kulielekeza gari upande ambao unateleza. Ukianfanikiwa kudhibiti gari, anza kulainisha magurudumu tena na kurejea barabarani. Hakikisha kwamba unabaki kuwa tulivu na usichukue hatua yoyote ghafla.
  12. Usiende kwa mwendo wa kasi. Iwapo una safari ya mbali, anza mapema kuhakikisha kwamba haukumbwi na shinikizo la kutaka kwenda kwa kasi ndipo ufike.
  13. Unapokuwa unaendesha gari, usishawishike kutumia simu yako au kufanya jambo lolote ambalo litakuzuia kuwa makini ukiliendesha gari.
  14. Iwapo utakuwa safarini, usiegeshe gari lako au kuanza kufanya shughuli zako karibu na mto wakati wa mvua.
  15. Ni vyema kusikiliza vituo vya redio na runinga kujifahamisha kuhusu yanayojiri na ni wapi mvua kubwaimenyesha au mafuriko kutokea.
  16. Usitembee kwenye maji au maeneo yenye matope ambayo kuna uwezekano kwamba kuna nyaya za umeme ambazo zimeanguka. Nyumba yako ikifurika maji pia, hakikisha umezima stima.
  17. Iwapo unatembea kwa miguu, tumia fimbo au kijiti kukadiria kina cha maji.
  18. Mafuriko yakitokea eneo ulipo, mara moja kimbilia maeneo yaliyo juu na salama. @BBC

Thursday, March 8, 2018

Maradhi ya fizi na meno.

Aina za maradhi ya fizi na dalili zake.

Kupiga mswaki na kutunza meno sio suala gumu na iwapo tutapiga mswaki ipaswavyo pamoja na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno, tunaweza kuzua maradhi ya fizi na pia meno kuoza. Maradhi ya fizi husababishwa na utando kwenye meno unaotengenezwa na bakteria, ute na chembechembe nyinginezo zinazoganda kwenye meno. Kwa mujibu wa Taasisi ya Meno ya Marekani (ADA) iwapo utando katika meno hautaondolewa huwa mgumu na kuwa ugwagwa wa meno au tarter inayotumiwa na bakteria. Mchanganyiko wa utando na ugwagwa katika meno husababisha uvimbe kwenye fizi hali inayojulikana kitaalamu kama gingivitis. Ukoga wa meno au ugwagwa unaweza kundolewe na daktari wa meno au dentist.
Maradhi ya fizi yana awamu tatu. Awamu ya kwanza kama tulivyosema ni gingivitis, ambapo fizi huwa nyukundu, huvimba na hutokwa na damu kwa urahisi. Iwapo hali hiyo itagundulika mapema inaweza kutatuliwa kwa kupiga mswaki vizuri na kutumia nyuzi kusafisha katikati ya meno.
Awamu ya pili ya ugonjwa wa fizi ni hali ijulikanayo kama Periodontitis ambapo uvimbe hutokea kuzunguka jino. Awamu hii ni iliyoendelea zaidi ya ugonjwa wa fizi inayotokea wakati sumu ya bakteria katika utando inapoharibu fizi zilizoshikilia jino. Suala hilo husababisha fizi ziachane na jino na kutengeneza mada haribifu. Baadhi ya wakati mfupa ulioliwa kuzunguka jino unaweza kuonekana. Matibabu ya maradhi haya ya fizi ni muhimu sana ili kuzuia mmomonyoko wa mfupa na kung'oka meno.
Awamu ya tatu ya maradhi ya fizi ni periodontitis iliyoendelea. Katika steji hii uharibifu wa fizi huwa mkubwa zaidi kuliko kabla na mfupa wa jino hulika. Pia meno huweza kung'oka na baadhi ya wakati huhitaji kung'olewa iwapo matibabu hayatosaidia.
Dalili za maradhi ya fizi
Hapa linajitokeza swali kwamba ni zipi dalili zinazojitokeza wakati mtu anapokuwa na ugonjwa wa fizi ulioendelea? Dalili za advanced periodontitis ni kuwa na harufu mbaya ya mdomo ambayo haiishi. Fizi kuvimba, kuwa nyekundu na laini. Dalili nyingine ni fizi kusogea mbali na meno, kuhisi maumivu wakati wa kutafuna na kupoteza hisia katika meno.
Sababu za maradhi ya fizi
Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kumfanya mtu awe katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya fizi. Miongoni mwa sababu hizo ni kuvuta sigara au kutafuna tumbaku. Mbali ya kuwa uvutaji sigara unaathiri mwili wa binadamu kwa njia tofauti, moja ya athari za ufutaji sigara hudhihirika katika kinywa cha mtu. Kwa kuwa moshi wa sigara hupita kwenye meno na fizi, kinywa cha mvuta sigara huwa kituo cha nicotine ambayo huharibu muonekano wa meno kwa kuyabadilisha rangi na kuacha harufu mbaya kinywani. Si hayo tu bali uvutaji sigara pia huathiri tishu za fizi na kupunguza mtiririko wa damu katika fizi, na kuleta uharibifu unaosababisha fizi zisogee mbali na meno.
Wataalamu wanatuarifu kuwa, asilimia 75 ya watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fizi ni watu wazima huku wale wanaovuta sigara wakiwa kwenye hatari ya kusumbuliwa na ugonjwa huo mara 7 zaidi ikilinganishwa na watu wasiovuta sigara.
Sababu nyingine inayochangia katika kupata ugonjwa wa fizi ni mabadiliko ya homoni kwa wasichana na wanawake. Wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya kinywa na meno kuliko wanaume kutokana na mabadiliko ya homoni yanayosababishwa na maumbile yao. Sio tu mabadiliko ya homoni kwa wanawake na watoto huathiri mtiririko wa damu katika tishu za fizi, bali pia huchangia katika suala zima la kupatikana ugando kwenye meno au plague unaosababisha meno kuoza. Mabadiliko ya homoni huwafanya wanawake wawe kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa fizi wanapokuwa katika hali tofauti kwenye maisha yao ambazo ni wakati wa kubalehe, wakati wa hedhi, wanapotumia vidonge vya kuzuia mimba, wanapokuwa wajawazito na wakati wanapoacha kupata hedhi yaani menopause.  Hayo yote husababishwa na mabadiliko yanayoshuhudiwa katika homoni za estrogen na progesterone kwenye vipindi hivyo.  Kwa sababu hiyo tunaweza kusema kuwa, watoto wa kike, wasichana na wanawake kwa ujumla wanapaswa kuzingatia zaidi usafi na utunzaji wa fizi na meno ili kuepusha uharibifu wa meno unaowapata zaidi kutokana na jinsia yao kuliko wanaume.
Sababu nyingine inayoweza kumfanya mtu apatwe na maradhi ya fizi ni ugonjwa wa kisukari. Madaktari wanatuambia kuwa, watu walio na ugonjwa wa kisukari ambao hawadhibiti vyema ugonjwa huo, wako katika hatari zaidi ya kupata matatizo ya meno na maambukizi katika fizi. Hii ni kwa sababu ugonjwa wa kisukari hupunguza mtiririko wa damu kwenye fizi na pia kiwango cha juu cha sukari kwenye damu husababisha kinywa kiwe kikavu na kuzidisha ugonjwa wa fizi. Upungufu wa mate mdomoni huongeza bakteria wanaoharibu meno na kuleta utando. Iwapo mtu mwenye kisukari atadhibiti ipasavyo kiwango cha sukari kwenye damu, hatari ya kupata matatizo ya meno hupungua.
Namna ya kuzuia maradhi ya fizi
Suala muhimu zaidi linaloweza kuzuia mtu asipatwe na maradhi ya fizi na kuoza meno ni kupiga mswaki na kutumia nyuzi kuondosha uchafu katikati ya meno kwa uchache mara moja kila siku. Suala hilo linaweza kuzuia maradhi ya fizi, meno kutoboka na kung'oka. Licha ya kusafisha meno kila siku, jambo jingine muhimu ni kufanyiwa uchunguzi na daktari wa meno kwa uchache mara moja kwa mwaka. Hii ni kwa sababu hata kama tunajitahidi kwa kiasi gani kupiga mswaki, lakini mgando na ugwagwa hujitokeza na kusababisha matatizo katika fizi.
Je, ni namna gani tupige mswaki kwa njia iliyo sahihi?
Kwanza kabisa tunashauriwa kupiga mswaki asubuhi na kabla ya kwenda kulala. Ikiwezekana piga mswaki baada ya kula chakula. Kama hauwezi, piga mswaki baada ya kula vyakula vya sukari. Tunapaswa kutumia mswaki laiini na wa wasitani, kwani mswaki mkubwa hautafika kwenye meno ya nyuma ilhali ule ulio mdogo utakufanya utumie wakati mwingi sana katika kusugua meno. Ikiwa unahitaji usaidizi katika kuchagua mswaki, pata ushauri kutoka kwa daktari wako wa meno. Tumia dawa ya meno iliyo na floraidi. Watoto wanapaswa kutumia kiasi kidogo cha dawa ya meno na watu wazima watie dawa ya meno kulingana na urefu wa nywele za mswaki.
Wataalamu wanatushauri kubadilisha mswaki pindi ule tunaotumia unapochoka, kila baada ya miezi mitatu au minne. Pia tunashauri kuwa ni vizuri kubadilisha mswaki mpya kila baada ya kupata mafua, uvimbe katika koo na magonjwa mengineyo kama hayo.
Kumbuka kusugua pande zote za meno kwa njia ifuatayo:
Sugua meno yako polepole bila kutumia nguvu kutoka sehemu ya nyuma hadi mbele. Sugua karibu na ufizi kwa mwendo wa mviringo, ili mswaki ufike sehemu ambapo meno na ufizi zinakutanika mahali ambako chembechembe za chakula hujificha.Sugua sehemu zote za meno, sehemu ya nje, sehemu ya kutafunia chakula na sehemu ya ndani ya meno.Tumia sehemu ya juu ya mswaki kusafisha sehemu ya ndani ya meno ya juu, kwa mwendo wa juu na chini.Sugua ulimi wako kwa upole ili kuondoa vijidudu au viini vinavyosababisha harufu mbaya.Sukutua na hifadhi mswaki wako sehemu nzuri na salama kwa matumizi ya baadaye.
Naaam wapenzi wasikilizaki, na kufikia hapo basi hatuna la ziada kwa leo, hadi wiki ijayo tudumishe afya zetu

DAWA 14 ZINAZOWEZA KUTIBU MAUMIVU YA GOTI

Gout au maumivu ya jongo kwa Kiswahili ni aina mojawapo ya maumivu ya mishipa na yanaweza kuleta maumivu makubwa katika maungio hasa katika kidole gumba cha mguu. Ishara kubwa za maumivu ya jongo ni maumivu ya uvimbe nyakati za usiku, kupatwa na hasira, na maumivu katika kidole kikubwa cha mguu. Unaweza pia kujisikia maumivu katika kifundo cha mguu, magotini au katika maungio mengine ya mwili.
Kitu kikubwa kinachosababisha maumivu ya jongo au gout ni kiasi kingi cha asidi katika mzunguko wa damu. Ikiwa unasikia maumivu kila mara katika mikono, vidole, magoti, katika maungio mbalimbali mwilini unashauriwa ukapate vipimo dhidi ya jongo.
Ukiacha maji ya kunywa ambayo ni mhimu sana katika kupunguza kiasi cha asidi mwilini, Hapa nimekuandikia mimea na matunda mhimu ambavyo vimejaribiwa na kuonyesha uwezo mkubwa katika kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

1.  Juisi ya limau

Juisi ya Limau ina viinilishe vya asili ambavyo vinaweza kusaidia kutibu maumivu ya jongo au gout kama tulivyozoea wengi wetu. Tafiti zinaonyesha kuwa matunda jamii ya chungwa kama vile machungwa yenyewe, machenza, na limau au ndimu husaidia kuyeyusha asidi iliyogandamana katika damu na hivyo kukupatia nafuu ya haraka itokanayo na maumivu ya gout. Tengeneza juisi hii ya limau ukichanganya na maji na unywe mara tatu kwa siku kwa majuma kadhaa.

2. Siki ya tufaha

Kwakuwa tunda la tufaha ni zuri katika kudhibiti gout hakuna shaka kwamba siki yake isiweze kudhibiti gout. Na kwa kawaida siki ya tufaha inafanya vizuri kutibu gout kuliko hata tunda lake. Siki ya tufaha ina asidi nzuri iitwayo acetic acid ambayo huongeza kiasi cha alkalini ndani ya mwili na kuunda usawa na mazingira mazuri ya pH (Potential Hydrogen) na hivyo moja kwa moja kuwa msaada mkubwa katika kupunguza na hata kutibu maumivu ya gout. Kumbuka pia hakuna utafiti ambao umefanywa kuthibitisha madai haya ya siki ya tufaha kuwa na uwezo huu. Unaweza kuchanganya siki ya tufaha katika chakula unachokula au kuongeza kijiko kikubwa kimoja katika glasi ya maji na unywe mara moja kila siku.

3. Baking Soda

Baking soda ina faida nyingi na matumizi mengi sana ikiwemo kukusaidia katika tatizo lako la gout. Sodium bicarbonate iliyomo kwenye baking soda huifanya damu kuwa na alkalini zaidi kitu ambacho ni mhimu katika kudhibiti gout. Chota kijiko kimoja kidogo cha baking soda na uiweke katika maji robo lita na unywe kutwa mara mbili kwa majuma kadhaa. Kama unasumbuliwa na shinikizo la juu la damu usiitumie hii baking soda kujitibu gout.

4.  Nanasi

Nanasi lina kimeng’enya mhimu kiitwacho ‘bromelain’ ambacho kina sifa ya kuzuia muwako wa ndani ya mwili (inflammation). Kwahiyo kuwa na mazoea ya kula nanasi kila siku kunaweza kuzuia usipatwe au hata kupunguza maumivu yatokanayo na gout.

5. Zabibu

Zabibu zina kiasi kingi cha kiuaji sumu na zinaweza kupunguza maumivu ya gout kwa haraka zaidi. Mbegu za tunda la zabibu zina kitu mhimu kiitwacho pycnogenolsambacho ni kiuaji sumu kingine kinachosaidia kupigana na aina zote za maumivu ya mishipa ikiwemo gout. Kula kila siku zabibu na utaona matokeo mazuri dhidi ya maumivu yako ya gout.

6. Tangawizi

Tangawizi ina matumizi mengi na imekuwa kwenye orodha ya dawa za asili au mbadala kwa ajili ya kutibu maradhi mengi kwa miaka mingi ikiwemo gout. Chemsha maji kama unachemsha maji ya chai, chukua tangawizi mbichi yaani ile ambayo siyo ya unga, kwangua (grate) kipande kimoja au viwili vya tangawizi ndani ya maji hayo yanayochemka, acha ichemke kama dakika 10, ipuwa na unywe kama chai kutwa mara tatu kwa wiki 3. Unaweza kuongeza asali au hata sukari kwenye huo mchanganyiko wa maji na tangawizi.

7. Ndizi

Ndizi zina kiasi kingi cha Potassiamu na Vitamini C na zinao uwezo pia wa kupunguza maumivu yatokanayo na gout kwa kuyeyusha asidi iliyoganda kwenye mkojo kuwa katika umajimaji ambao mwili wako unaweza kuutoa nje kirahisi. Kula ndizi kila mara kama unasumbuliwa na gout.

8. Mcheri

Tunda la mcheri lina kiasi kingi cha Vitamini C ambayo ni msaada mkubwa katika kupunguza asidi katika damu. Matunda 20 ya mcheri yakiliwa katika vipindi tofauti tofauti katika siku yanaweza kufanya maajabu dhidi ya maumivu yako ya gout. Ukinywa juisi ya mcheri pia ina matokeo yaliyo sawa na ukila matunda yake.

9. Unga wa mkaa

Pengine tayari unajuwa kuwa mkaa unao uwezo wa kuondoa harufu mbaya na hata sumu mwilini. Lakini lile ulikuwa hujuwi hadi sasa ni kuwa unga wa mkaa ambao unapatikana kwa kuusaga tu mkaa, unaweza pia kupunguza maumivu yatokanayo na gout.
Changanya unga huu wa mkaa katika maji, chukua kitambaa kilichotengenezwa kwa pamba na ukiloweke kwenye hayo maji kisha funika katika eneo lenye maumivu ukiacha hapo kwa dakika kadhaa mara kwa mara kwa siku kwa majuma kadhaa kutasaidia kama siyo kuondoa kabisa maumivu ya gout.

10. Maji ya Kunywa

Maji ni mhimu sana katika kushusha maumivu ya kwenye maungio ikiwemo gout. Maji ndicho kilainishi mhimu katika viungo vyote vya mwili. Kunywa kila siku glasi 8 mpaka 10 za maji, maji yaliyo katika joto la kawaida na siyo ya baridi, ukifanya hivi kila siku baada ya wiki 2 au 3 utakuwa huru kabisa na maumivu ya gout.

11. Juisi ya maharage machanga (French Beans)

Kunywa Juisi hii ya maharage machanga kwa muda wa mwezi mmoja ili kupata matokeo mazuri. Shida itakuwa namna ya kuyapata haya maharage hasa kwa wale walio nje ya D’salaam lakini ukihitaji nijulishe.

12. Mharadali

Mharadali (Mustard) ni nzuri sana katika kupunguza maumivu ya gout. Chukuwa mharadali ya unga na uweke kwenye eneo lenye maumivu na uuache ufyonzwe na ngozi yako kwa usiku mzima na utakapoamka asubuhi utajisikia vizuri kabisa.

13. Mchanganyiko wa juisi ya matunda na mboga mboga
Mchanganyiko wa juisi ya tango, magimbi na karoti unawea kutumika kutuliza maumivu yatokanayo na gout haraka sana.

14. Mafuta ya nyonyo

Pasha kidogo mafuta ya nyonyo katika moto kisha pakaa eneo lenye maumivu taratibu kama vile unafanya masaji kwa dakika kadhaa mara mbili mpaka tatu kwa siku, fanya hivi kila siku mpaka utakapopona kabisa.